Kutoka kwa Abdillah bin Mas'udi -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: Amesema M…
Islam > Sw > Hadith > Fiqhi ya tabia > Kutoka kwa Abdillah bin Mas'udi -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: Amesema M…
Hadith imesimuliwa na: Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Sahihi
Mis à jour le 26 octobre 2026
📖 1 min de lecture
Maandishi ya hadith: Kutoka kwa Abdillah bin Mas'udi -radhi za Mwenyezi Mung…
Maelezo ya hadith: Kutoka kwa Abdillah bin Mas'udi -radhi za Mwenyezi Mung…
Mtume rehema na amani ziwe juu yake ameamrisha ukweli, na akasema kuwa kushikamana nao kunapelekea katika matendo mema ya kudumu, na mwenye kushikamana na kufanya wema humpeleka mtendaji wake Peponi, na ukweli wake unapoendelea mara kwa mara kwa siri na hadharani, basi hustahiki jina la mkweli; nayo ni sifa ya hali ya juu zaidi ya ukweli. Kisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake akaonya dhidi ya kusema uongo na kusema maneno ya batili; Kwa sababu inawachochea watu kuacha uadilifu, na kufanya maovu, ufisadi, na dhambi, kisha inawapeleka Motoni, na anapoendelea kukithirisha kusema uongo basi mpaka huandikwa kwa Mwenyezi Mungu kuwa ni miongoni mwa waongo.
Mafunzo: Kutoka kwa Abdillah bin Mas'udi -radhi za Mwenyezi Mung…
- Ukweli ni tabia adhimu ambayo hupatikana kupitia juhudi, kwa sababu mtu anapoendelea kuwa mkweli na kuutafuta ukweli, mpaka ukweli unakuwa ni kama tabia yake ya asili, basi huandikwa mbele ya Mwenyezi Mungu kuwa ni miongoni mwa wa watu wakweli na wema.
- Uongo ni tabia ya kulaumiwa ambayo mhusika huipata kupitia mazoea ya muda mrefu katika maneno na matendo, mpaka inakuwa ni tabia na silika yake, kisha anaandikwa mbele ya Mwenyezi Mungu kuwa ni katika waongo.
- Ukweli unahusu ukweli wa ulimi, ambao ni kinyume cha uongo, na ukweli katika nia, ambao ni ikhlasi, na ukweli katika kusuluhisha vyema nia yake, na ukweli katika vitendo, na kwa uchache zaidi ni siri yake na dhahiri yake viwe sawa, na ukweli katika matukio kama kusema ukweli wakati wa hofu na raha, na mengineyo, hivyo yeyote atakayesifika na sifa hizo basi atakuwa ni mkweli mno, au akasifika na baadhi yake atakuwa mkweli pia.
Makundi :
Fiq'hi ya Tabia.
· Tabia njema.
· Mambo mazuri na Adabu- Heshima.
بسم الله الرحمن الرحيم
mar. 15 Joumada 1
الثلاثاء 15 جمادى الأولى
أستغفر الله
Je demande pardon à Allah