Islam > Sw > Hadith > Mambo mazuri na adabu heshima > Hakika katika wabora wenu ni mtu mwenye tabia njema kuliko wote
SahihiMis à jour le 26 octobre 2026
📖 1 min de lectureعن عبد الله بن عمرو رضي الله عنهما قال: لَمْ يَكُنِ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَاحِشًا وَلَا مُتَفَحِّشًا، وَكَانَ يَقُولُ: «إِنَّ مِنْ خِيَارِكُمْ أَحْسَنَكُمْ أَخْلَاقًا».
Haikuwa katika tabia za Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa na maneno machafu, au vitendo vibaya, na hakuwa anayataka hayo wala kuyatafuta kwa makusudi, basi Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- ni mwenye tabia tukufu.
Na alikuwa -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: Hakika mbora wenu mbele ya Allah ni mwenye tabia nzuri zaidi kuliko wote, kwa kutenda wema, na kuwa na uso mkunjufu, na kuacha maudhi na kuyavumilia, na kujichanganya pamoja na watu kwa yale mazuri.
Makundi : Fiq'hi ya Tabia. · Tabia njema. · Mambo mazuri na Adabu- Heshima.