Hakuna msaada na riziki mnayopewa nyinyi isipokuwa ni kupitia kwa watu madhaifu wenu
Islam > Sw > Hadith > Tungo zenye kulainisha moyo na mawaidha > Hakuna msaada na riziki mnayopewa nyinyi isipokuwa ni kupitia kwa watu madhaifu wenu
Hadith imesimuliwa na: Imepokelewa na Al-Bukhaariy
Sahihi
Mis à jour le 26 octobre 2026
📖 1 min de lecture
Maandishi ya hadith: Hakuna msaada na riziki mnayopewa nyinyi isipokuwa ni k…
Maelezo ya hadith: Hakuna msaada na riziki mnayopewa nyinyi isipokuwa ni k…
Alidhania Saadi bin Abii Waqas radhi za Allah ziwe juu yake kuwa yeye ana ubora kuliko aliye chini yake katika watu madhaifu, kwa sababu ya ushujaa wake na mfano wa hilo!. Akasema rehema na amani ziwe juu yake: Tambueni kuwa hamnusuriwi wala hampewi riziki isipokuwa kwa watu wenu madhaifu kwa dua zao na swala zao na utakasifu wao wa nia; kwani wao mara nyingi ndio hutakasa dua zaidi, na huwa na unyenyekevu zaidi katika ibada kwa sababu nyoyo zao ziko tupu hazifungamani na mapambo ya dunia.
Mafunzo: Hakuna msaada na riziki mnayopewa nyinyi isipokuwa ni k…
- Himizo la kuwa mnyenyekevu na katazo la kujiona bora kwa watu wengine.
- Amesema bin Hajari: Ikiwa mwenye nguvu anakuwa na hadhi kwa ubora wa ushujaa wake, basi mtu dhaifu anakuwa bora kwa dua yake na utakasifu wa nia yake (Ikhlas yake).
- Himizo la kutenda wema kwa mafakiri na kuwapa haki zao, kwani hilo ni katika sababu za kupata rehema ya Mwenyezi Mungu kwako na msaada wake.
Makundi :
Tungo zenye kulainisha moyo na mawaidha
· Hali za watu wema.
· Mambo mazuri na Adabu- Heshima.
بسم الله الرحمن الرحيم
mer. 16 Joumada 1
الأربعاء 16 جمادى الأولى
الله أكبر
Allah est le plus grand