Ninamuapa Mwenyezi Mungu, ikiwa Mwenyezi Mungu atamuongoza mtu mmoja kupitia kwako, hilo n…

Islam > Sw > Hadith > Tiba na kutumia dawa na ruqya ya kisheria > Ninamuapa Mwenyezi Mungu, ikiwa Mwenyezi Mungu atamuongoza mtu mmoja kupitia kwako, hilo n…

Hadith imesimuliwa na: Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake

Sahihi

Mis à jour le 26 octobre 2026

📖 2 min de lecture

Maandishi ya hadith: Ninamuapa Mwenyezi Mungu, ikiwa Mwenyezi Mungu atamuong…

Maelezo ya hadith: Ninamuapa Mwenyezi Mungu, ikiwa Mwenyezi Mungu atamuong…

Mtume rehema na amani ziwe juu yake aliwaeleza Maswahaba kuhusu ushindi wa Waislamu dhidi ya Mayahudi wa Khaibar siku ya kesho, na hilo litakuwa mikononi mwa mtu atakayempa bendera, nayo ni bendera ambayo hutumiwa na jeshi kama nembo yake. Na mtu huyu miongoni mwa sifa zake ni pamoja na kumpenda Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na Mwenyezi Mungu na Mtume wake wanampenda. Kwa hiyo Maswahaba walipitisha usiku kucha wakijadiliana na kuzungumza juu ya nani atapewa bendera? Kwa kutamani kuipata heshima hii kubwa, Ilipofika asubuhi walikwenda kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake wote wakiwa na matumaini ya kupata heshima hii.

Basi Mtume rehema na amani ziwe juu yake akamuulizia Ally bin Abi Twalib Allah amuwie radhi?

Pakasemwa: Ni mgonjwa na analalamika kuhusu macho yake.

Basi rehema na amani zimshukie, akamtumia watu wakamlete, akamtemea Ally machoni katika mate yake matukufu na akamuombea, akapona ugonjwa wake kana kwamba hakuwa na maradhi, akampa bendera na akamwamuru aende kwa upole mpaka aikaribie ngome ya maadui na awaite katika Uislamu, ikiwa watamjibu; Awaambie ni wajibu gani wanapaswa kufanya.

Kisha rehema na amani ziwe juu yake, akamueleza Ally ubora wa kumuita mtu kwa Mwenyezi Mungu, na kwamba ikiwa mlinganiaji atakuwa ni sababu ya kuongoka kwa mtu mmoja, hiyo ni bora zaidi kwake kuliko kuwa na ngamia wekundu ambao ndio utajiri wa thamani zaidi kwa Waarabu, azimiliki au azitoe sadaka.

Mafunzo: Ninamuapa Mwenyezi Mungu, ikiwa Mwenyezi Mungu atamuong…

Makundi : Tiba na kutumia dawa na Ruq'ya ya kisheria. · Mambo yaliyo bora. · Ubora wa Maswahaba Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao. · Historia ya Mtume. · Fiq'hi na misingi yake. · Vita alivyoshiriki na Ambavyo hajashiriki Mtume Rehema na amani za Allah ziwe juu yake: · Mambo mazuri na Adabu- Heshima. · Historia na Taarekh.

بسم الله الرحمن الرحيم mar. 15 Joumada 1
الثلاثاء 15 جمادى الأولى
بدر Pleine Lune Jour 16.5 / 29.5
Illumination 97%
Nouvelle lune dans 13 jours
الله أكبر Allah est le plus grand

إِنَّ ٱللَّهَ وَمَلَٰٓئِكَتَهُۥ يُصَلُّونَ عَلَى ٱلنَّبِىِّ ۚ يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ صَلُّوا۟ عَلَيْهِ وَسَلِّمُوا۟ تَسْلِيمًا

Al-Ahzab 33:56