Hakika makombe, na hirizi, na limbwata, ni ushirikina

Islam > Sw > Hadith > Fiqhi na misingi yake > Hakika makombe, na hirizi, na limbwata, ni ushirikina

Hadith imesimuliwa na: Imepokelewa na Abu Daud, Ibn Majah na Ahmad

Sahihi

Mis à jour le 26 octobre 2026

📖 1 min de lecture

Maandishi ya hadith: Hakika makombe, na hirizi, na limbwata, ni ushirikina

عن عبد الله بن مسعود رضي الله عنه قال: سمعت رسول الله صلى الله عليه وسلم يقول: «إنَّ الرُّقَى والتَمائِمَ والتِّوَلَةَ شِرْكٌ».

Maelezo ya hadith: Hakika makombe, na hirizi, na limbwata, ni ushirikina

Amebainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- vitu ambavyo kuvifanya kwake ni katika ushirikina; na miongoni mwavyo ni:

Cha kwanza: Makombe: Ni maneno ambayo watu wajinga huyatumia kama tiba yanayoambatana na ushirikina.

Cha pili: Vyenye kutundikwa ni kama hirizi na mfano wake: zinazotundikwa kwa watoto wadogo na wanyama na wengineo kwa ajili ya kuzuia kijicho.

Cha tatu: Limbwata: Ambalo hutengenezwa ili mmoja kati ya wanandoa amvute mwenzake kimapenzi.

Mambo haya yote ni katika ushirikina: Kwa sababu hii ni katika kukifanya kitu kuwa sababu, hali yakuwa si sababu ya kisheria iliyothibiti kwa ushahidi, wala si sababu inayoonekana wazi iliyothibiti kwa majaribio. Ama sababu za kisheria kama kusoma Qur'ani, au zenye kuonekana kama dawa zilizothibiti kwa majaribio, hizi zinafaa pamoja na kuamini kuwa hizi ni sababu tu, nakuwa manufaa na madhara yako mkononi mwa Mwenyezi Mungu.

Mafunzo: Hakika makombe, na hirizi, na limbwata, ni ushirikina

Makundi : Tiba na kutumia dawa na Ruq'ya ya kisheria. · Ruq'ya ya Kisheria. · Fiq'hi na misingi yake.

بسم الله الرحمن الرحيم mar. 15 Joumada 1
الثلاثاء 15 جمادى الأولى
بدر Pleine Lune Jour 16.5 / 29.5
Illumination 97%
Nouvelle lune dans 13 jours
سبحان الله Gloire à Allah

إِنَّ ٱللَّهَ وَمَلَٰٓئِكَتَهُۥ يُصَلُّونَ عَلَى ٱلنَّبِىِّ ۚ يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ صَلُّوا۟ عَلَيْهِ وَسَلِّمُوا۟ تَسْلِيمًا

Al-Ahzab 33:56