Islam > Sw > Hadith > Akida itikadi > Alifariki Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- hali yakuwa hakuna chochote nyumbani kwake…
SahihiMis à jour le 26 octobre 2026
📖 1 min de lectureعن عائشة رضي الله عنها قالت: تُوُفِّيَ رسول الله صلى الله عليه وسلم وما في بيتي من شيء يَأكُلُهُ ذُو كَبدٍ إلا شَطْرُ شَعير في رَفٍّ لي، فأكَلتُ منه حتى طال عليَّ، فَكِلْتُهُ فَفَنِيَ.
Anaeleza Aisha -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- kuwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- alifariki hali yakuwa hakuna nyumbani kwake chochote isipokuwa kiasi kidogo cha ngano, na maana yake ni kiwango kidogo cha ngano, kama alivyoifasiri imamu Tirmidhiy, akaendelea kula katika chakula alichokiacha Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- kwa muda mrefu, alipokipima kikamalizika, na hii ni ishara ya kuendelea kwa baraka zake -Rehema na Amani ziwe juu yake- katika chakula hicho kidogo, pamoja na kutokuwepo kwa kipimo kinachoonyesha kiasi wakati wa kumtegemea Mwenyezi Mungu, kipimo wakati wa kuuziana kinahitajika kwaajili ya kuweka sawa haki ya wale wenye kuuziana, ama kipimo wakati wa kutoa sadaka haipendezi (si katika sunna).
Makundi : Akida- Itikadi- · Historia ya Mtume. · Wake zake Mtume Rehema na amani za Allah ziwe juu yake na hali ya Nyumba ya Mtume. · Kuamini mitume · Historia na Taarekh. · Mtume wetu Muhammad - Rehema na amani za Allah ziwe juu yake-