Enyi watu hakika Mwenyezi Mungu ameondosha kwenu nyinyi kiburi cha zama za ujinga, na kuji…

Islam > Sw > Hadith > Quran tukufu na elimu zake > Enyi watu hakika Mwenyezi Mungu ameondosha kwenu nyinyi kiburi cha zama za ujinga, na kuji…

Hadith imesimuliwa na: Imepokelewa na Tirmidhi na bin Hibban

Sahihi

Mis à jour le 26 octobre 2026

📖 1 min de lecture

Maandishi ya hadith: Enyi watu hakika Mwenyezi Mungu ameondosha kwenu nyinyi…

عَنِ ‌ابْنِ عُمَرَ رضي الله عنهما: أَنَّ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ خَطَبَ النَّاسَ يَوْمَ فَتْحِ مَكَّةَ، فَقَالَ: «يَا أَيُّهَا النَّاسُ، إِنَّ اللهَ قَدْ أَذْهَبَ عَنْكُمْ عُبِّيَّةَ الْجَاهِلِيَّةِ وَتَعَاظُمَهَا بِآبَائِهَا، فَالنَّاسُ رَجُلَانِ: بَرٌّ تَقِيٌّ كَرِيمٌ عَلَى اللهِ، وَفَاجِرٌ شَقِيٌّ هَيِّنٌ عَلَى اللهِ، وَالنَّاسُ بَنُو آدَمَ، وَخَلَقَ اللهُ آدَمَ مِنْ تُرَابٍ، قَالَ اللهُ: {يَا أَيُّهَا النَّاسُ إِنَّا خَلَقْنَاكُمْ مِنْ ذَكَرٍ وَأُنْثَى وَجَعَلْنَاكُمْ شُعُوبًا وَقَبَائِلَ لِتَعَارَفُوا إِنَّ أَكْرَمَكُمْ عِنْدَ اللهِ أَتْقَاكُمْ إِنَّ اللهَ عَلِيمٌ خَبِيرٌ} [الحجرات: 13]».

Maelezo ya hadith: Enyi watu hakika Mwenyezi Mungu ameondosha kwenu nyinyi…

Aliwahutubia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- watu siku ya ufunguzi wa mji wa Makka akasema: Enyi watu! Hakika Mwenyezi Mungu amenyanyua na akaondosha kwenu nyinyi kiburi cha zama za ujinga na kujiona, na kujifaharisha kwa baba zenu (nasaba), bali watu wako aina mbili:

Ni ima muumini mwema, mchamungu, mtiifu, mwenye kumuabudu Mwenyezi Mungu Mtukufu, huyu ni mtukufu mbele ya Mwenyezi Mungu, hata kama hana cheo au nasaba nzuri mbele za watu.

Na ima kafiri muovu, na huyu ni dhalili kwa Mwenyezi Mungu, na wala hana thamani yoyote, hata kama ana ukoo mzuri na cheo na mamlaka.

Na watu wote ni watoto wa Adam, na Mwenyezi Mungu kamuumba Adam kutokana na udongo, haifai kwa kiumbe ambaye asili yake ni udongo kuwa na kiburi na kujiona yeye ni bora, na hili linasadikishwa na kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Enyi watu! hakika sisi tumekuumbeni nyinyi kutokana na mwanaume na mwanamke na tukakufanyeni kuwa mataifa na makabila ili mpate kujuana, hakika mbora wenu mbele ya Mwenyezi Mungu ni mchamungu wenu, hakika Mwenyezi Mungu ni mjuzi na ana habari (ya myafanyayo) [Alhujrat:13].

Mafunzo: Enyi watu hakika Mwenyezi Mungu ameondosha kwenu nyinyi…

Makundi : Qur'an tukufu na Elimu zake · Tafsiri ya Qur'an. · Kulingania na kuelekeza kwa Mungu. · Ubora wa uislamu na uzuri wake. · Kuenea kwa dini ya uislamu. · Haki za Mwanadamu katika uislamu · Da'awa na (kujitolea) kuamrisha mema na kukataza mabaya · Tafsiri za Aya

بسم الله الرحمن الرحيم mar. 15 Joumada 1
الثلاثاء 15 جمادى الأولى
بدر Pleine Lune Jour 16.5 / 29.5
Illumination 96%
Nouvelle lune dans 13 jours
سبحان الله Gloire à Allah

إِنَّ ٱللَّهَ وَمَلَٰٓئِكَتَهُۥ يُصَلُّونَ عَلَى ٱلنَّبِىِّ ۚ يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ صَلُّوا۟ عَلَيْهِ وَسَلِّمُوا۟ تَسْلِيمًا

Al-Ahzab 33:56