Wameangamia wenye kufanya uzito katika mambo
Islam > Sw > Hadith > Akida itikadi > Wameangamia wenye kufanya uzito katika mambo
Hadith imesimuliwa na: Imepokelewa Imamu Muslim
Sahihi
Mis à jour le 26 octobre 2026
📖 1 min de lecture
Maandishi ya hadith: Wameangamia wenye kufanya uzito katika mambo
عن عبد الله بن مسعود قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: «هَلَكَ الْمُتَنَطِّعُون» قالها ثلاثًا.
Maelezo ya hadith: Wameangamia wenye kufanya uzito katika mambo
Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuhusu kufeli na kupata hasara kwa watiao ugumu -pasina uongofu wala kuwa na elimu- katika dini yao na dunia yao, na katika kauli zao na matendo yao, wenye kuvuka mipaka ya sheria aliyokuja nayo Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-.
Mafunzo: Wameangamia wenye kufanya uzito katika mambo
- Uharamu wa misimamo mikali katika mambo yote, na himizo la kuepuka hilo katika kila kitu; hasa hasa katika ibada na kuwatukuza watu wema.
- Kutafuta ukamilifu katika ibada na mengine mazuri; na kunakuwa kwa kufuata sheria.
- Inapendeza kulitilia mkazo jambo muhimu, kwa sababu Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alikariri sentensi hii mara tatu.
- Upole wa uislamu na wepesi wake.
Makundi :
Akida- Itikadi-
· Kumuamini Allah mwenye nguvu aliye tukuka
· Kumpwekesha Mwenyezi Mungu kwa Uungu wake.
بسم الله الرحمن الرحيم
mar. 15 Joumada 1
الثلاثاء 15 جمادى الأولى
سبحان الله وبحمده
Gloire et louange à Allah