Hakuna kuambukizana maradhi, wala kutuhumu mikosi kwa sababu ya ndege, na kinachonipendeza…

Islam > Sw > Hadith > Akida itikadi > Hakuna kuambukizana maradhi, wala kutuhumu mikosi kwa sababu ya ndege, na kinachonipendeza…

Hadith imesimuliwa na: Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake

Sahihi

Mis à jour le 26 octobre 2026

📖 1 min de lecture

Maandishi ya hadith: Hakuna kuambukizana maradhi, wala kutuhumu mikosi kwa s…

عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ رضي الله عنه عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «لَا عَدْوَى، وَلَا طِيَرَةَ، وَيُعْجِبُنِي الْفَأْلُ» قَالَ قِيلَ: وَمَا الْفَأْلُ؟ قَالَ: «الْكَلِمَةُ الطَّيِّبَةُ».

Maelezo ya hadith: Hakuna kuambukizana maradhi, wala kutuhumu mikosi kwa s…

Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa kuambukizana ambako walikuwa wakiamini watu wa zama za ujinga kuwa maradhi yanahama yenyewe kwenda kwa mwingine pasina kadari ya Mwenyezi Mungu, nikuwa madai hayo ni batili, nakuwa mikosi ya ndege ni batili, nayo ni mikosi kupitia kitu chochote chenye kuhisika au kuonekana, kama ndege au wanyama, au walemavu, au namba au siku au kinginecho, hapa ametaja ndege kwa sababu ni kitendo kilichokuwa maarufu zama za ujinga, na asili yake ilikuwa ni kumuachia ndege wakati wa kuanza kazi yoyote, kama safari au biashara au kinginecho, akiruka kuelekea kushoto mtu anaamini ni mkosi, na anaahirisha alichotaka kukifanya. Kisha akaeleza -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa anafurahishwa sana na mtu kujipa matumaini, nayo ni mtu kuwa na furaha na raha, kwa maneno mazuri anayoyasikia, yatakayomfanya awe na dhana nzuri na Mola wake Mlezi.

Mafunzo: Hakuna kuambukizana maradhi, wala kutuhumu mikosi kwa s…

Makundi : Akida- Itikadi- · Kumuamini Allah mwenye nguvu aliye tukuka · Kumpwekesha Mwenyezi Mungu kwa Uungu wake.

بسم الله الرحمن الرحيم mar. 15 Joumada 1
الثلاثاء 15 جمادى الأولى
بدر Pleine Lune Jour 16.6 / 29.5
Illumination 96%
Nouvelle lune dans 13 jours
اللهم صل على محمد Ô Allah prie sur Muhammad

إِنَّ ٱللَّهَ وَمَلَٰٓئِكَتَهُۥ يُصَلُّونَ عَلَى ٱلنَّبِىِّ ۚ يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ صَلُّوا۟ عَلَيْهِ وَسَلِّمُوا۟ تَسْلِيمًا

Al-Ahzab 33:56