Mwenye kukitegemea kitu hufungamanishwa kwacho
Islam > Sw > Hadith > Akida itikadi > Mwenye kukitegemea kitu hufungamanishwa kwacho
Hadith imesimuliwa na: Imepokelewa na Imamu Tirmidhiy - Imepokelewa na Ahmad
Ni nzuri
Mis à jour le 26 octobre 2026
📖 1 min de lecture
Maandishi ya hadith: Mwenye kukitegemea kitu hufungamanishwa kwacho
عن عبد الله بن عكيم رضي الله عنه مرفوعاً: «مَنْ تَعَلَّقَ شيئا وُكِلَ إليه».
Maelezo ya hadith: Mwenye kukitegemea kitu hufungamanishwa kwacho
Atakayegeuka kwa moyo wake au vitendo vyake au kwa vyote viwili katika kitu ambacho anataraji manufaa au kuzuia madhara, Mwenyezi Mungu humuwakilisha katika kitu hicho ambacho amekielekea, atakayemuelekea Mwenyezi Mungu humtosheleza na humfanyia wepesi kila zito, na mwenye kumuelekea asiyekuwa yeye Mwenyezi Mungu humfungamanisha katika kitu hicho na humfedhehesha.
Mafunzo: Mwenye kukitegemea kitu hufungamanishwa kwacho
- Katazo la kuegemea kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu.
- Ulazima wa kuegemea kwa Mwenyezi Mungu katika mambo yote.
- Kubainishwa madhara ya ushirikina na ubaya wa mwisho wake.
- Malipo huendana na matendo.
- Nikuwa malipo ya kitendo hurudi kwa mfanyaji yakiwa ya kheri au ya shari.
- Kushindwa kwa mwenye kujiondoa kwa Mwenyezi Mungu na akatafuta manufaa kwa asiyekuwa yeye.
Makundi :
Tungo zenye kulainisha moyo na mawaidha
· Akida- Itikadi-
· Matendo ya moyoni.
· Mambo mazuri na Adabu- Heshima.
· Kumuamini Allah mwenye nguvu aliye tukuka
· Kumpwekesha Mwenyezi Mungu kwa Uungu wake.
بسم الله الرحمن الرحيم
mer. 16 Joumada 1
الأربعاء 16 جمادى الأولى
لا حول ولا قوة إلا بالله
Pas de force ni de puissance sauf en Allah