Laiti Dunia ingelingana na ubawa wa mbu kwa thamani yake mbele ya Allah mtukufu basi kafir…

Islam > Sw > Hadith > Mambo mazuri na adabu heshima > Laiti Dunia ingelingana na ubawa wa mbu kwa thamani yake mbele ya Allah mtukufu basi kafir…

Hadith imesimuliwa na: Imepokelewa na Imamu Tirmidhiy

Sahihi

Mis à jour le 26 octobre 2026

📖 1 min de lecture

Maandishi ya hadith: Laiti Dunia ingelingana na ubawa wa mbu kwa thamani yak…

عن سهل بن سعد الساعدي ـرضي الله عنه- قَالَ رَسُول اللَّه -صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم-: «لو كانت الدنيا تَعدل عند الله جَناح بَعوضة، ما سَقَى كافراً منها شَرْبَة ماء».

Maelezo ya hadith: Laiti Dunia ingelingana na ubawa wa mbu kwa thamani yak…

Katika hadithi kumebainishwa udhalili wa Dunia kwa Mwenyezi Mungu -Mtukufu- nakuwa haina thamani, na lau ingekuwa hata na thamani ndogo zaidi kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu basi asingemnywesha kafiri hata funda moja ya maji, achilia mbali kule kuneemeka kwake nayo na kustareheka na mambo yake mazuri, Hivyo ikawa dunia ni dhalili mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, tofauti na Akhera, kwani hiyo ni nyumba ya neema za kudumu kwa watu wenye imani na ni maalumu kwaajili yao kinyume na makafiri, hivyo inawapasa watu wenye imani wajue uhalisia wa hii dunia na wasiiegemee, kwani ni nyumba ya kupita na si nyumba ya kudumu, wachukue ndani yake yale yatakayowasidia Akhera ambayo ndiyo nyumba ya kudumu. Amesema Mtukufu: "Na hakuna chochote mlichopewa basi hicho ni starehe ya dunia na pambo lake, na yaliyo kwa Mwenyezi Mungu ndiyo bora na ni yenye kubakia, hivi hamzingatii, hivi kwani tuliyemuahidi ahadi nzuri naye atakutana nayo anaweza kuwa sawa na tuliyemstarehesha starehe za maisha ya dunia kisha yeye siku ya kiyama atakuwa ni miongoni mwa wenye kuhudhurishwa".

Makundi : Tungo zenye kulainisha moyo na mawaidha · Kuyasema vibaya mapenzi ya kuipenda dunia. · Mambo mazuri na Adabu- Heshima.

بسم الله الرحمن الرحيم mar. 15 Joumada 1
الثلاثاء 15 جمادى الأولى
بدر Pleine Lune Jour 16.5 / 29.5
Illumination 97%
Nouvelle lune dans 13 jours
لا إله إلا الله Pas de divinité sauf Allah

إِنَّ ٱللَّهَ وَمَلَٰٓئِكَتَهُۥ يُصَلُّونَ عَلَى ٱلنَّبِىِّ ۚ يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ صَلُّوا۟ عَلَيْهِ وَسَلِّمُوا۟ تَسْلِيمًا

Al-Ahzab 33:56