Ama mimi sikukuapisheni kwa sababu ya kuwatuhumu, lakini Jibril alinijia na kuniambia kuwa…

Islam > Sw > Hadith > Mambo mazuri na adabu heshima > Ama mimi sikukuapisheni kwa sababu ya kuwatuhumu, lakini Jibril alinijia na kuniambia kuwa…

Hadith imesimuliwa na: Imepokelewa Imamu Muslim

Sahihi

Mis à jour le 26 octobre 2026

📖 2 min de lecture

Maandishi ya hadith: Ama mimi sikukuapisheni kwa sababu ya kuwatuhumu, lakin…

عَنْ أَبِي سَعِيدٍ الْخُدْرِيِّ قَالَ: خَرَجَ مُعَاوِيَةُ عَلَى حَلْقَةٍ فِي الْمَسْجِدِ، فَقَالَ: مَا أَجْلَسَكُمْ؟ قَالُوا: جَلَسْنَا نَذْكُرُ اللهَ، قَالَ آللَّهِ مَا أَجْلَسَكُمْ إِلَّا ذَاكَ؟ قَالُوا: وَاللهِ مَا أَجْلَسَنَا إِلَّا ذَاكَ، قَالَ: أَمَا إِنِّي لَمْ أَسْتَحْلِفْكُمْ تُهْمَةً لَكُمْ، وَمَا كَانَ أَحَدٌ بِمَنْزِلَتِي مِنْ رَسُولِ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَقَلَّ عَنْهُ حَدِيثًا مِنِّي: وَإِنَّ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ خَرَجَ عَلَى حَلْقَةٍ مِنْ أَصْحَابِهِ، فَقَالَ: «مَا أَجْلَسَكُمْ؟» قَالُوا: جَلَسْنَا نَذْكُرُ اللهَ وَنَحْمَدُهُ عَلَى مَا هَدَانَا لِلْإِسْلَامِ، وَمَنَّ بِهِ عَلَيْنَا، قَالَ: «آللَّهِ مَا أَجْلَسَكُمْ إِلَّا ذَاكَ؟» قَالُوا: وَاللهِ مَا أَجْلَسَنَا إِلَّا ذَاكَ، قَالَ: «أَمَا إِنِّي لَمْ أَسْتَحْلِفْكُمْ تُهْمَةً لَكُمْ، وَلَكِنَّهُ أَتَانِي جِبْرِيلُ فَأَخْبَرَنِي أَنَّ اللهَ عَزَّ وَجَلَّ يُبَاهِي بِكُمُ الْمَلَائِكَةَ».

Maelezo ya hadith: Ama mimi sikukuapisheni kwa sababu ya kuwatuhumu, lakin…

Alitoka Muawia bin Abi Sufian, Mwenyezi Mungu awawie radhi, kwenda katika kundi moja msikitini na akawauliza wamekusanyika kwa jambo gani, Wakasema: Tunamtaja Mwenyezi Mungu, basi akawaapisha, Mwenyezi Mungu awe radhi naye, kwamba hawakutaka katika kikao chao na mkusanyiko wao isipokuwa ni kumtaja Mwenyezi Mungu, wakaapa kwa hilo, kisha akawaambia: Sikukuapisheni kwa tuhuma yoyote juu yenu au kuwa na shaka juu ya ukweli wenu, kisha akaeleza kuhusu hali yake kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake na kwamba hakuna aliyekuwa karibu naye kuliko yeye. Kwa sababu Ummu Habiba alikuwa ni dada yake, mke wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na kwa sababu alikuwa ni miongoni mwa waandishi wa wahyi, lakini ilikuwa ni nadra sana kusimulia hadithi, Basi akawaambia kuwa Mtume, rehema na amani ziwe juu yake, siku moja alitoka nyumbani kwake na akawakuta wamekaa msikitini wakimdhukuru Mwenyezi Mungu na kumhimidi kwa yale aliyowaongoza katika Uislamu na kuwakirimia. Mwenyezi Mungu amfikishie rehema na amani, akawauliza na kuwaapisha sawa na alivyofanya Muawia kwa jamaa zake, Mwenyezi Mungu amuwie radhi. Kisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake akawaambia kuhusu sababu ya kuwauliza kwake na kuapa kwao: kwamba Malaika Jibril, amani iwe juu yake, alimjia na kumwambia kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu anajifakhirisha kupitia nyinyi kwa Malaika, na anawadhihirishia ubora wenu na anawaonyesha uzuri wa amali yenu, na anakusifieni mbele yao.

Mafunzo: Ama mimi sikukuapisheni kwa sababu ya kuwatuhumu, lakin…

Makundi : Mambo yaliyo bora. · Ubora wa Elimu. · Fadhila za Adh-kaar. · Mambo mazuri na Adabu- Heshima.

بسم الله الرحمن الرحيم mar. 15 Joumada 1
الثلاثاء 15 جمادى الأولى
بدر Pleine Lune Jour 16.5 / 29.5
Illumination 96%
Nouvelle lune dans 13 jours
سبحان الله وبحمده Gloire et louange à Allah

إِنَّ ٱللَّهَ وَمَلَٰٓئِكَتَهُۥ يُصَلُّونَ عَلَى ٱلنَّبِىِّ ۚ يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ صَلُّوا۟ عَلَيْهِ وَسَلِّمُوا۟ تَسْلِيمًا

Al-Ahzab 33:56