Islam > Sw > Hadith > Akida itikadi > Hakika hao wawili wanaadhibiwa, na hawaadhibiwi kwa makosa makubwa, ama mmoja wao alikuwa …
SahihiMis à jour le 26 octobre 2026
📖 1 min de lectureعَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ رضي الله عنهما قَالَ: مَرَّ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ بِقَبْرَيْنِ، فَقَالَ: «إِنَّهُمَا لَيُعَذَّبَانِ، وَمَا يُعَذَّبَانِ فِي كَبِيرٍ، أَمَّا أَحَدُهُمَا فَكَانَ لاَ يَسْتَتِرُ مِنَ البَوْلِ، وَأَمَّا الآخَرُ فَكَانَ يَمْشِي بِالنَّمِيمَةِ» ثُمَّ أَخَذَ جَرِيدَةً رَطْبَةً، فَشَقَّهَا نِصْفَيْنِ، فَغَرَزَ فِي كُلِّ قَبْرٍ وَاحِدَةً، قَالُوا: يَا رَسُولَ اللَّهِ، لِمَ فَعَلْتَ هَذَا؟ قَالَ: «لَعَلَّهُ يُخَفِّفُ عَنْهُمَا مَا لَمْ يَيْبَسَا».
Alipita Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- katika makaburi mawili akasema: Hakika watu wa makaburi haya mawili wanaadhibiwa; na wala hawaadhibiwa katika jambo kubwa, hata kama ni kubwa mbele ya Mwenyezi Mungu, Ama mmoja wao alikuwa hajali katika kuhifadhi mwili wake na nguo zake kutokana na mkojo anapokidhi haja yake, Na mwingine alikuwa akitembea kati ya watu kwa uchonganishi, akinukuu maneno ya mtu mwingine kwa lengo la kuwadhuru na kuleta sintofahamu baina yao na ugomvi kati ya watu.
Makundi : Fiq'hi ya Tabia. · Tungo zenye kulainisha moyo na mawaidha · Tabia mbovu. · Akida- Itikadi- · Watu wa makaburini. · Mambo mazuri na Adabu- Heshima. · Kuamini siku ya mwisho · Maisha ya Barzakhi (Baada ya kufa)