Msiyafanye majumba yenu kuwa makaburi, na wala msilifanye kaburi langu kuwa sikukuu, na ni…
Islam > Sw > Hadith > Mambo mazuri na adabu heshima > Msiyafanye majumba yenu kuwa makaburi, na wala msilifanye kaburi langu kuwa sikukuu, na ni…
Hadith imesimuliwa na: Imepokelewa na Abu Daud
Ni nzuri (Hasan)
Mis à jour le 26 octobre 2026
📖 1 min de lecture
Maandishi ya hadith: Msiyafanye majumba yenu kuwa makaburi, na wala msilifan…
عن أبي هريرة رضي الله عنه قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: «لَا تَجْعَلُوا بُيُوتَكُمْ قُبُورًا، وَلَا تَجْعَلُوا قَبْرِي عِيدًا، وَصَلُّوا عَلَيَّ؛ فَإِنَّ صَلَاتَكُمْ تَبْلُغُنِي حَيْثُ كُنْتُمْ».
Maelezo ya hadith: Msiyafanye majumba yenu kuwa makaburi, na wala msilifan…
Anakataza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- majumba kubaki tupu bila ibada ya swala ndani yake, yakawa kama makaburi ambayo hayaswaliwi ndani yake, Na akakataza kurudi mara kwa mara kutembelea kaburi lake na kukusanyika hapo kwa namna ya mazoea; kwani hilo ni njia ya kuelekea katika ushirikina, Na akaamrisha kumtakia rehema na amani juu yake mahala popote katika uso wa ardhi; kwani dua hizo humfikia kutoka kwa aliyekaribu na aliyembali kwa kiwango sawa, haina haja ya kurudi mara kwa mara katika kaburi lake.
Mafunzo: Msiyafanye majumba yenu kuwa makaburi, na wala msilifan…
- Katazo la kuziacha nyumba bila ya kumuabudia Allah Mtukufu ndani ya majumba hayo.
- Katazo la kufunga safari kwa ajili ya kuzuru kaburi la Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-; kwani yeye aliamrisha kumuombea rehema juu yake na akaeleza kuwa zinamfikia, bali hufungwa safari kwa kuukusudia msikiti pekee na kusali ndani yake.
- Uharamu wa kulifanyia matembezi kaburi la Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa ni sikukuu, kwa kukithirisha kulizuru kwa namna maalum na kwa nyakati maalum, na vile vile ziara ya kaburi lolote.
- Utukufu wa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kwa Mola wake, kwa kuwekwa sheria ya kumtakia rehema kwa kila zama na kila mahali.
- Kiasi kwamba katazo la kuswali makaburini limepitishwa kwa maswahaba; kwa ajili hii alikataza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- majumba kufanywa kuwa kama makaburi hakusaliwi ndani yake.
Makundi :
Mambo yaliyo bora.
· Ubora na fadhila za matendo mema.
· Mambo mazuri na Adabu- Heshima.
بسم الله الرحمن الرحيم
mar. 15 Joumada 1
الثلاثاء 15 جمادى الأولى
سبحان الله وبحمده
Gloire et louange à Allah