Wakikutana waislamu wawili kwa mapanga yao, basi muuaji na muuliwaji wote motoni
Islam > Sw > Hadith > Mambo mazuri na adabu heshima > Wakikutana waislamu wawili kwa mapanga yao, basi muuaji na muuliwaji wote motoni
Hadith imesimuliwa na: Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Sahihi
Mis à jour le 26 octobre 2026
📖 1 min de lecture
Maandishi ya hadith: Wakikutana waislamu wawili kwa mapanga yao, basi muuaji…
عن أبي بَكرة رضي الله عنه قال: سمعت رسول الله صلى الله عليه وسلم يقول: «إِذَا الْتَقَى الْمُسْلِمَانِ بِسَيْفَيْهِمَا فَالْقَاتِلُ وَالْمَقْتُولُ فِي النَّارِ»، فَقُلْتُ: يَا رَسُولَ اللهِ هَذَا الْقَاتِلُ، فَمَا بَالُ الْمَقْتُولِ؟ قَالَ: «إِنَّهُ كَانَ حَرِيصًا عَلَى قَتْلِ صَاحِبِهِ».
Maelezo ya hadith: Wakikutana waislamu wawili kwa mapanga yao, basi muuaji…
Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa wakikutana waislamu wawili kwa mapanga yao, akiwa na dhamira kila mmoja wao ya kummaliza mwenzake; Basi muuaji motoni kwa sababu ya kutekeleza mauaji ya kumuua mwenzake, Kuhusu muuliwaji, hilo likamtatiza Swahaba: Ni vipi anakuwa motoni? Akaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa hata yeye pia anakuwa motoni kwa sababu ya pupa yake ya kumuua mwenzake, na hakikumzuia kuuwa zaidi ya muuaji kumuwahi na kummaliza.
Mafunzo: Wakikutana waislamu wawili kwa mapanga yao, basi muuaji…
- Anastahiki adhabu mwenye kukusudia madhambi kwa moyo wake na akazifanya sababu zake.
- Tahadhari kali ya kutopigana waislamu kwa waislamu, na kuna ahadi ya moto.
- Mapigano kati ya waislam kwa haki hayaingii katika ahadi hii ya adhabu, mfano kama kuwapiga vita waasi na mafisadi.
- Mwenye kutenda dhambi kubwa hakufuru kwa kulifanya pekee; Kwa sababu Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kawaita wenye kupigana kuwa ni waislamu.
- Watakapokutana waislamu wawili kwa nyenzo yoyote miongoni mwa nyenzo za kuuwana, mmoja akamuunza mwenzake, basi muuwaji na muuliwaji wote motoni, na kutajwa panga katika hadithi ni sehemu ya mfano tu.
Makundi :
Tungo zenye kulainisha moyo na mawaidha
· Matendo ya moyoni.
· Kuyasema vibaya Maasi.
· Mambo mazuri na Adabu- Heshima.
بسم الله الرحمن الرحيم
mar. 15 Joumada 1
الثلاثاء 15 جمادى الأولى
اللهم صل على محمد
Ô Allah prie sur Muhammad