Islam > Sw > Hadith > Mambo mazuri na adabu heshima > Ipe nyongo dunia Allah atakupenda ,na usivitolee macho vitu vya watu, watu watakupenda
Amesema Imamu Nawawi: Hadithi hii ni hasanMis à jour le 26 octobre 2026
📖 1 min de lectureعَنْ أَبِي العَبَّاسِ سَهْلِ بْنِ سَعِدٍ السَّاعِدِيِّ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ: جَاءَ رَجُلٌ إِلَى النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَقَالَ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، دُلَّنِي عَلَى عَمَلٍ إِذَا عَمِلْتُهُ أَحَبَّنِي اللَّهُ وَأَحَبَّنِي النَّاسُ، فَقَالَ: «ازْهَدْ فِي الدُّنْيَا يُحِبُّكَ اللَّهُ، وَازْهَدْ فِيمَا عِنْدَ النَّاسِ يُحِبُّكَ النَّاسُ».
Mtu mmoja alimuuliza Mtume rehema na amani ziwe juu yake amuelekeze katika amali ambayo akiifanya Mwenyezi Mungu atampenda na watu watampenda, Mtume rehema na amani ziwe juu yake akasema kumwambia: Atakupenda Mwenyezi Mungu utakapoacha yasiyo na msingi katika Dunia, na yale yasiyokunufaisha katika Akhera, na ukaacha yale yanayoweza kuwa na madhara katika dini yako, na watu watakupenda utakapoyapa nyongo yaliyoko mikononi mwao miongoni mwa vitu vya kidunia; kwa sababu wanayapenda kulingana na tabia zao za asili, na atakayebanana nao katika hayo watamchukia, na atakayewaachia watampenda.
Makundi : Tungo zenye kulainisha moyo na mawaidha · Kuipa nyongo Dunia na Kujiepusha na yaliyo haramu. · Mambo mazuri na Adabu- Heshima.