Hivi mnajua ni nini kusengenya?", Wakasema: Mwenyezi Mungu na Mtume wake ndio wajuzi, akas…
Islam > Sw > Hadith > Mambo mazuri na adabu heshima > Hivi mnajua ni nini kusengenya?", Wakasema: Mwenyezi Mungu na Mtume wake ndio wajuzi, akas…
Hadith imesimuliwa na: Imepokelewa Imamu Muslim
Sahihi
Mis à jour le 26 octobre 2026
📖 1 min de lecture
Maandishi ya hadith: Hivi mnajua ni nini kusengenya?", Wakasema: Mwenyezi Mu…
عن أبي هريرة رضي الله عنه أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال: «أَتَدْرُونَ مَا الْغِيبَةُ؟»، قَالُوا: اللهُ وَرَسُولُهُ أَعْلَمُ، قَالَ: «ذِكْرُكَ أَخَاكَ بِمَا يَكْرَهُ»، قِيلَ: أَفَرَأَيْتَ إِنْ كَانَ فِي أَخِي مَا أَقُولُ؟ قَالَ: «إِنْ كَانَ فِيهِ مَا تَقُولُ فَقَدِ اغْتَبْتَهُ، وَإِنْ لَمْ يَكُنْ فِيهِ فَقَدْ بَهَتَّهُ».
Maelezo ya hadith: Hivi mnajua ni nini kusengenya?", Wakasema: Mwenyezi Mu…
Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- ukweli kuhusu kusengenya kuliko haramishwa, nako ni: Kumsema muislamu asiyekuwepo kwa yale anayoyachukia, sawa sawa iwe ni katika sifa zake za kimaumbile au za kitabia, mfano: Chongo, mpiga ghushi, muongo, na mfano wa hayo katika sifa mbaya, hata kama sifa hizo anazo.
Ama zisipokuwa kwake sifa hizo hii ndio mbaya zaidi kuliko kusengenya, nako ni kuzua uongo, yaani: kumzulia mtu asiyokuwa nayo.
Mafunzo: Hivi mnajua ni nini kusengenya?", Wakasema: Mwenyezi Mu…
- Uzuri wa mafundisho ya Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kiasi kwamba hutoa mafundisho kwa njia ya swali.
- Uzuri wa adabu ya Masahaba wakiwa pamoja na Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, waliposema: Mwenyezi Mungu na Mtume ndio wajuzi.
- Kauli ya muulizwaji kwa lile asilolijua: Mwenyezi Mungu ndiye Mjuzi zaidi.
- Sheria imelinda jamii, na imehifadhi haki na udugu baina yao.
- Kusengenya ni haramu isipokuwa katika baadhi ya hali kwa ajili ya masilahi; Na miongoni mwake: Ni kuzuia dhulma, kiasi kwamba atamtaja aliyedhulumiwa yule aliyemdhulumu kwa yule anayeweza kumchukulia haki yake, akasema: Fulani kanidhulumu, au kanifanyia jambo hili na lile, ikiwemo pia kutaka ushauri katika swala la kuoa au ushirika au ukaribu, na mfamo wake.
Makundi :
Adabu za kisheria.
· Adabu za mazungumzo na kunyamaza.
· Mambo mazuri na Adabu- Heshima.
بسم الله الرحمن الرحيم
mar. 15 Joumada 1
الثلاثاء 15 جمادى الأولى
اللهم صل على محمد
Ô Allah prie sur Muhammad