Islam > Sw > Hadith > Mambo mazuri na adabu heshima > Ilikuwa Dua aiombayo zaidi Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake-:ni "Ewe Mola wetu Mlezi…
SahihiMis à jour le 26 octobre 2026
📖 1 min de lectureعَنْ أَنَسٍ رضي الله عنه قَالَ: كَانَ أَكْثَرُ دُعَاءِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «اللَّهُمَّ رَبَّنَا آتِنَا فِي الدُّنْيَا حَسَنَةً، وَفِي الآخِرَةِ حَسَنَةً، وَقِنَا عَذَابَ النَّارِ».
Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akikithirisha dua kwa dua fupi zenye kukusanya mambo mengi, na miongoni mwake: "Ewe Mwenyezi Mungu! Tupe hapa katika Dunia (mambo) mazuri, na Akhera utupe mazuri na utukinge na adhabu ya moto", Dua hii inakusanya mazuri yote ya Dunia; ikiwemo riziki ya raha na pana na ya halali, na mke mwema, na mtoto kitulizo cha jicho, na starehe, na elimu yenye manufaa, na mfano wa hayo miongoni mwa maombi yanayopendeka na ya halali, na mazuri ya Akhera ni kusalimika na adhabu za kaburi, na kisimamo cha Kiyama na moto, na kupata radhi za Mwenyezi Mungu, na kufaulu kwa kupata neema za kudumu, na kuwekwa karibu na Mola Mlezi Mwingi wa huruma.
Makundi : Fiq'hi -Elimu- ya Dua na Dhikri mbali mbali. · Dua zilizopokelewa toka kwa mtume. · Mambo mazuri na Adabu- Heshima.