Hamshukuru Mwenyezi Mungu asiyewashukuru watu
Islam > Sw > Hadith > Fiqhi ya tabia > Hamshukuru Mwenyezi Mungu asiyewashukuru watu
Hadith imesimuliwa na: Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy na Ahmad
Sahihi
Mis à jour le 26 octobre 2026
📖 1 min de lecture
Maandishi ya hadith: Hamshukuru Mwenyezi Mungu asiyewashukuru watu
Maelezo ya hadith: Hamshukuru Mwenyezi Mungu asiyewashukuru watu
Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa kwa kawaida hamshukuru Mwenyezi Mungu asiyewashukuru watu kwa wema na mazuri waliyomfanyia, na hii ni kwa sababu mambo haya mawili yote yanaungana, kiasi kwamba katika tabia yake na desturi yake ni kukufuru neema na kuacha kushukuru, pia atakuwa katika kawaida yake ni kukufuru neema za Mwenyezi Mungu na kupuuza katika kushukuru kwa neema hizo.
Mafunzo: Hamshukuru Mwenyezi Mungu asiyewashukuru watu
- Umuhimu wa kuwashukuru watu kwa mazuri.
- Mneemeshaji halisia ni Mwenyezi Mungu Mtukufu, na viumbe ni sababu, huileta Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa amtakaye, na kwa hivyo kuwashukuru watu ni miongoni mwa kumshukuru Mwenyezi Mungu Mtukufu.
- Kuwashukuru watu kwa wema ni dalili ya ukamilifu wa tabia njema.
Makundi :
Fiq'hi ya Tabia.
· Tabia njema.
· Mambo mazuri na Adabu- Heshima.
بسم الله الرحمن الرحيم
mer. 16 Joumada 1
الأربعاء 16 جمادى الأولى
لا حول ولا قوة إلا بالله
Pas de force ni de puissance sauf en Allah