Huenda mwenye nywele timtimu mwenye kusukumwa katika milango, lau angeliapia kwa Mwenyezi …
Islam > Sw > Hadith > Mambo yaliyo bora > Huenda mwenye nywele timtimu mwenye kusukumwa katika milango, lau angeliapia kwa Mwenyezi …
Hadith imesimuliwa na: Imepokelewa Imamu Muslim
Sahihi
Mis à jour le 26 octobre 2026
📖 1 min de lecture
Maandishi ya hadith: Huenda mwenye nywele timtimu mwenye kusukumwa katika mi…
Maelezo ya hadith: Huenda mwenye nywele timtimu mwenye kusukumwa katika mi…
Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kwamba kuna baadhi ya watu wana nywele zilizoshikana tena zilizojaa vumbi, na hawazipaki mafuta wala hajali kuziosha, na wala hawana heshima yoyote mbele za watu, basi watu humsukuma mtu kama huyu katika milango yao, na kumfukuza kwa kumdharau; isipokuwa mtu huyu lau angeapa kwa Mwenyezi Mungu kuwa litokee jambo basi Mwenyezi Mungu angelitenda jambo hilo kwa sababu ya kumkirimu na kumtukuza kwa kujibu ombi lake, na kumlinda asijekupotoka katika kiapo chake, na hii ni kwa sababu ya ubora wake na nafasi yake mbele ya Mwenyezi Mungu.
Mafunzo: Huenda mwenye nywele timtimu mwenye kusukumwa katika mi…
- Mwenyezi Mungu hatazami sura ya mja, lakini anatazama ndani ya nyoyo na matendo.
- Ni jukumu la kila mtu kuyapa kipaumbele matendo yake na usafi wa moyo wake zaidi kuliko kuutilia maanani mwili wake na mavazi yake.
- Kujinyenyekeza kwa Mwenyezi Mungu na kujidhalilisha kwake ni sababu ya kujibiwa dua, na ndiyo maana; Mwenyezi Mungu hukiepusha kuanguka patupu kiapo cha wachamungu na wenye maisha duni.
- Kumebainishwa malezi ya kiutume kwa watu; ili wasidharauliane wao kwa wao.
Makundi :
Mambo yaliyo bora.
· Ubora na fadhila za matendo mema.
· Mambo mazuri na Adabu- Heshima.
بسم الله الرحمن الرحيم
mar. 15 Joumada 1
الثلاثاء 15 جمادى الأولى
لا حول ولا قوة إلا بالله
Pas de force ni de puissance sauf en Allah