Enyi watu, tubieni kwa Mwenyezi Mungu, kwani mimi ninatubia kwa siku mara mia moja
Islam > Sw > Hadith > Mambo yaliyo bora > Enyi watu, tubieni kwa Mwenyezi Mungu, kwani mimi ninatubia kwa siku mara mia moja
Hadith imesimuliwa na: Imepokelewa Imamu Muslim
Sahihi
Mis à jour le 26 octobre 2026
📖 1 min de lecture
Maandishi ya hadith: Enyi watu, tubieni kwa Mwenyezi Mungu, kwani mimi ninat…
Maelezo ya hadith: Enyi watu, tubieni kwa Mwenyezi Mungu, kwani mimi ninat…
Anawaamrisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake watu kukithirisha kuomba toba na msamaha, na anajielezea mwenyewe kuwa yeye hutubia kwa Mwneyezi Mungu Mtukufu na kumuomba msamaha kwa siku zaidi ya mara mia moja, na haliyakuwa alikwisha samehewa yaliyotangulia katika madhambi yake na yajayo, na katika hilo kuna ukamilifu wa kujidhalilisha kwa Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka.
Mafunzo: Enyi watu, tubieni kwa Mwenyezi Mungu, kwani mimi ninat…
- Kila mmoja vyovyote itakavyokuwa nafasi yake na daraja lake katika imani, basi anahitaji kurejea kwa Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka, na kuikamilisha nafsi yake kwa toba, nakuwa kila mmoja hakosi mapungufu katika kutimiza haki za Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka: "Na tubieni kwa Mwenyezi Mungu nyote enyi waumini".
- Toba ni kwa mambo yote, sawa sawa kwa kufanya maharamisho au madhambi au uzembe katika kutimiza wajibu.
- Ikhlasi (kutakasa nia) katika toba ni sharti la kukubaliwa kwake, atakayeacha dhambi kwa ajili ya asiyekuwa Mwenyezi Mungu huyo bado hajatubia.
- Amesema Nawawi: Toba ina masharti matatu: Ajivue katika maasi, na ajute kwa kuyafanya, na atie dhamira ya kweli ya kutorudi katika maasi mfano wake kabisa, na ikiwa maasi yanahusiana na haki ya binadamu basi kuna sharti la nne, nalo: Kurudisha haki aliyodhulumu kwa mwenye nayo, na kujivua nayo.
- Tahadhari: Kuomba msamaha kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake hakuna maana kuwa kuna madhambi aliyafanya, lakini ni kwa sababu ya ukamilifu wa utumwa wake na kufungamana kwake na kumtaja Aliyetakasika na kutukuka, na kuvuta kwake taswira ya utukufu wa haki ya Mwenyezi Mungu Mtukufu na upungufu wa mja kwa namna yoyote atakayofanya katika kushukuru neema zake, nayo inakuwa ni sehemu ya kuwawekea sheria umma wake baada yake, na hukumu zinginezo.
Makundi :
Mambo yaliyo bora.
· Fiq'hi -Elimu- ya Dua na Dhikri mbali mbali.
· Fadhila za Adh-kaar.
· Muongozo wa Mtume Rehema na Amani za Allah ziwe juu yake katika kuleta Adh-kaar- nyiradi.
· Mambo mazuri na Adabu- Heshima.
بسم الله الرحمن الرحيم
mar. 15 Joumada 1
الثلاثاء 15 جمادى الأولى
لا إله إلا الله
Pas de divinité sauf Allah