Nilisema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, ni nani nimfanyie wema zaidi? Akasema: "Mama yako,…
Islam > Sw > Hadith > Mambo yaliyo bora > Nilisema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, ni nani nimfanyie wema zaidi? Akasema: "Mama yako,…
Hadith imesimuliwa na: Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy na Ahmad
Ni nzuri (Hasan)
Mis à jour le 26 octobre 2026
📖 1 min de lecture
Maandishi ya hadith: Nilisema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, ni nani nimfany…
Maelezo ya hadith: Nilisema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, ni nani nimfany…
Amebainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa mtu muhimu zaidi kufanyiwa wema kuliko wote, na kumfanyia hisani, na kuamiliana naye vizuri, na kuishi naye vizuri, na kusuhubiana naye na kumuunga: Ni mama, na akasisitiza haki ya mama zaidi kuliko mtu mwingine, kwa kulirudia hilo mara tatu; kwa kubainisha fadhila zake kuliko watu wengine bila kupunguza chochote. Kisha akasema rehema na amani ziwe juu yake anayefuata katika kutendewa wema: Kisha baba, kisha ndugu wa karibu zaidi na wa karibu anayefuata, kila ndugu anavyozidi kuwa karibu basi anakuwa na haki zaidi ya kuungwa udugu kuliko ndugu wa mbali.
Mafunzo: Nilisema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, ni nani nimfany…
- Mazungumzo haya ni katika kumtanguliza mama, kisha baba, kisha ndugu wa karibu zaidi na wa karibu anayefuata, kulingana na daraja zao katika ukaribu.
- Kumebainishwa nafasi ya wazazi wawili na hasa hasa mama.
- Amekariri katika hadithi wema kwa mama mara tatu; na hii ni kwa sababu ya ukubwa wa fadhila yake kwa watoto wake, na kwa sababu ya wingi wa matatizo anayovumilia na tabu na uzito wa ujauzito, kisha kujifungua, kisha kunyonyesha, mambo ambayo yako kwake pekee, kisha baba anashiriki katika malezi.
Makundi :
Mambo yaliyo bora.
· Ubora wa Kuwatendea Wema wazazi wawili:
· Mambo mazuri na Adabu- Heshima.
بسم الله الرحمن الرحيم
mar. 15 Joumada 1
الثلاثاء 15 جمادى الأولى
لا إله إلا الله
Pas de divinité sauf Allah