Ubora wa msomi kwa mchamungu, ni kama ubora wangu mimi kwa aliyechini yenu

Islam > Sw > Hadith > Mambo yaliyo bora > Ubora wa msomi kwa mchamungu, ni kama ubora wangu mimi kwa aliyechini yenu

Hadith imesimuliwa na: Imepokelewa Imamu Tirmidhiy

Ni nzuri kwa sababu ya hadithi nyinginezo

Mis à jour le 26 octobre 2026

📖 1 min de lecture

Maandishi ya hadith: Ubora wa msomi kwa mchamungu, ni kama ubora wangu mimi…

Maelezo ya hadith: Ubora wa msomi kwa mchamungu, ni kama ubora wangu mimi…

Walitajwa watu wawili kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake mmoja wao ni mchamungu, na mwingine msomi, ni yupo mbora kati yao?

Akasema rehema na amani ziwe juu yake: Ubora wa msomi wa elimu ya kisheria mwenye kuifanyia kazi na mwenye kuifundisha kwa mchamungu aliyejitenga kwa ajili ya ibada, pamoja na kujua kwake yale ya wajibu kwake katika elimu ni kama ubora wake rehema na amani ziwe juu yake na utukufu wake kwa Swahaba wa chini zaidi. Kisha akabainisha rehema na amani ziwe juu yake sababu ya hilo, kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu, na Malaika wake miongoni mwa wabeba Arshi, na wakazi wa mbinguni katika Malaika wengineo, na wakazi wa Ardhi kwanzia binadam na majini na wanyama wote, hata mdudu chungu katika makazi yake ndani ya tumbo la Ardhi, na hata nyangumi na samaki wa Baharini; alitaja hivi ili waingie katika kauli hii viumbe wa nchi kavu na Baharini, wote hawa wanamuombea mazuri mwenye kuwafundisha watu elimu ya dini ambayo ndani yake kuna uokovu wa watu na mafanikio yao.

Mafunzo: Ubora wa msomi kwa mchamungu, ni kama ubora wangu mimi…

Makundi : Mambo yaliyo bora. · Ubora wa Elimu. · Mambo mazuri na Adabu- Heshima.

بسم الله الرحمن الرحيم mer. 16 Joumada 1
الأربعاء 16 جمادى الأولى
أحدب متناقص Gibbeuse Décroissante Jour 16.6 / 29.5
Illumination 96%
Nouvelle lune dans 13 jours
الله أكبر Allah est le plus grand

إِنَّ ٱللَّهَ وَمَلَٰٓئِكَتَهُۥ يُصَلُّونَ عَلَى ٱلنَّبِىِّ ۚ يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ صَلُّوا۟ عَلَيْهِ وَسَلِّمُوا۟ تَسْلِيمًا

Al-Ahzab 33:56