Naona ndoto zenu zimeafikiana katika siku saba za mwisho, basi atakayetaka kuitafuta basi …
Islam > Sw > Hadith > Fiqhi ufahamu wa ibada mbalimbali > Naona ndoto zenu zimeafikiana katika siku saba za mwisho, basi atakayetaka kuitafuta basi …
Hadith imesimuliwa na: Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Sahihi
Mis à jour le 26 octobre 2026
📖 1 min de lecture
Maandishi ya hadith: Naona ndoto zenu zimeafikiana katika siku saba za mwish…
Maelezo ya hadith: Naona ndoto zenu zimeafikiana katika siku saba za mwish…
Wanaume katika Maswahaba wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake waliona ndotoni kuwa Lailatul Qadri inakuwa katika siku saba za mwisho wa Ramadhani. Akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Ninaona ndoto zenu zimeafikiana katika siku saba za mwisho wa Ramadhani, atakayeitaka, akiwa na pupa ya kuitafuta, basi ajitahidi kuiwinda na kuitafuta kwa kukithirisha matendo mema kwani inatarajiwa zaidi kuwa katika siku saba za mwisho, nazo zinaanza kwanzia usiku wa tarehe ishirini na nne mwezi wa Ramadhani unapokuwa na siku thelathini, na zinaanza usiku wa tarehe thelathini na tatu mwezi unapokuwa wa siku ishirini na tisa.
Mafunzo: Naona ndoto zenu zimeafikiana katika siku saba za mwish…
- Ubora wa Lailatul-Qadri na himizo la kuitafuta.
- Miongoni mwa hekima za Mwenyezi Mungu na huruma yake aliuficha usiku huu ili watu waongeze juhudi katika ibada, kwa ajili ya kuutafuta, ili zikithiri thawabu zao.
- Usiku wa Lailatul-Qadri uko katika siku kumi za mwisho wa Ramadhani, na katika siku saba za mwisho ndio hutarajiwa zaidi.
- Usiku wenye cheo ni moja kati ya siku za kumi la mwisho la Ramadhani, nao ndio usiku ambao Mwenyezi Mungu aliiteremsha Qur'ani ndani yake kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na akaufanya usiku huu kuwa ni bora kuliko miezi elfu moja katika baraka zake, na utukufu wa heshima yake, na athari ya matendo mema ndani yake.
- Umeitwa kuwa ni usiku wa Lailatul-Qadri, kwa kuiwekea sakna dali, ima ni kwa sababu ya utukufu wake, husemwa: Fulani anacheo kikubwa, inakuwa kuuambatanisha usiku ni katika sehemu ya kuambatanisha kitu katika sifa yake, yaani usiku mtukufu, yaani unacheo kikubwa kwa utukufu na thamani na nafasi mpaka mwisho wake, "Hakika sisi tumeiteremsha katika usiku wenye baraka" [Ad-Dukhan: 3]. Na ima imetokana na kukadiria: Inakuwa kuambatanishwa kwake ni kuambatanishwa kwa kiambata na kile kinachokizunguka, yaani ni usiku ambao ndani yake kunakuwa na makadirio ya yale yatakayoendelea katika mwaka mzima, "Katika usiku huu hubainishwa kila jambo la hekima" [Ad-Dukhan: 4].
Makundi :
Fiq'hi- Ufahamu- wa Ibada mbalimbali.
· Funga.
· Fiq'hi na misingi yake.
· Masiku kumi ya mwisho wa mwezi wa Ramadhani.
بسم الله الرحمن الرحيم
mar. 15 Joumada 1
الثلاثاء 15 جمادى الأولى
حسبنا الله ونعم الوكيل
Allah nous suffit, quel excellent protecteur