Hakika matendo yote huzingatiwa nia, na hakika kila mtu hulipwa kwa lile alilonuia

Islam > Sw > Hadith > Mambo mazuri na adabu heshima > Hakika matendo yote huzingatiwa nia, na hakika kila mtu hulipwa kwa lile alilonuia

Hadith imesimuliwa na: Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake

Sahihi

Mis à jour le 26 octobre 2026

📖 1 min de lecture

Maandishi ya hadith: Hakika matendo yote huzingatiwa nia, na hakika kila mtu…

عن عمر بن الخطاب رضي الله عنه قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: «إِنَّمَا الْأَعْمَالُ بِالنِّيَّةِ، وَإِنَّمَا لِامْرِئٍ مَا نَوَى، فَمَنْ كَانَتْ هِجْرَتُهُ إِلَى اللهِ وَرَسُولِهِ، فَهِجْرَتُهُ إِلَى اللهِ وَرَسُولِهِ، وَمَنْ كَانَتْ هِجْرَتُهُ لِدُنْيَا يُصِيبُهَا أَوِ امْرَأَةٍ يَتَزَوَّجُهَا، فَهِجْرَتُهُ إِلَى مَا هَاجَرَ إِلَيْهِ».
وفي لفظ للبخاري: «إِنَّمَا الْأَعْمَالُ بِالنِّيَّاتِ، وَإِنَّمَا لِكُلِّ امْرِئٍ مَا نَوَى».

Maelezo ya hadith: Hakika matendo yote huzingatiwa nia, na hakika kila mtu…

Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa matendo yote huzingatiwa nia, na hukumu hii ni ya ujumla katika amali zote, kwanzia ibada na miamala, atakaye kusudia kupata masilahi katika amali yake hatopata zaidi ya masilahi na wala hatopata thawabu, na atakayekusudia katika amali yake kujiweka karibu na Allah Mtukufu, atapata thawabu na malipo kupitia amali yake hata kama litakuwa ni jambo la kawaida, kama kula na kunywa.

Kisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akapiga mfano wa kuweka wazi namna gani nia inaathiri matendo pamoja nakuwa huonekana yote yako sawa katika muonekano wa juu, akaweka wazi kuwa atakayekusudia katika kuhama kwake na kuacha nchi yake ni kutafuta radhi za Mola wake, basi kuhama kwake kutakuwa ni kwa kisheria na kunakubalika, atalipwa kwa sababu ya ukweli wa nia yake, na atakayekusudia kwa kuhama kwake ni kupata masilahi ya kidunia, kama mali, au cheo, au mke, basi hatopata kwa kuhama kwake huko zaidi ya manufaa aliyoyakusudia, na wala hatokuwa na fungu la malipo na thawabu.

Mafunzo: Hakika matendo yote huzingatiwa nia, na hakika kila mtu…

Makundi : Tungo zenye kulainisha moyo na mawaidha · Matendo ya moyoni. · Mambo mazuri na Adabu- Heshima.

بسم الله الرحمن الرحيم mer. 16 Joumada 1
الأربعاء 16 جمادى الأولى
أحدب متناقص Gibbeuse Décroissante Jour 16.6 / 29.5
Illumination 96%
Nouvelle lune dans 13 jours
سبحان الله Gloire à Allah

إِنَّ ٱللَّهَ وَمَلَٰٓئِكَتَهُۥ يُصَلُّونَ عَلَى ٱلنَّبِىِّ ۚ يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ صَلُّوا۟ عَلَيْهِ وَسَلِّمُوا۟ تَسْلِيمًا

Al-Ahzab 33:56