Msiwatukane wafu, kwani wao tayari wameyapata yale waliyoyatanguliza
Islam > Sw > Hadith > Fiqhi na misingi yake > Msiwatukane wafu, kwani wao tayari wameyapata yale waliyoyatanguliza
Hadith imesimuliwa na: Imepokelewa na Al-Bukhaariy
Sahihi
Mis à jour le 26 octobre 2026
📖 1 min de lecture
Maandishi ya hadith: Msiwatukane wafu, kwani wao tayari wameyapata yale wali…
عن عائشة رضي الله عنها قالت: قال النبي صلى الله عليه وسلم: «لَا تَسُبُّوا الْأَمْوَاتَ، فَإِنَّهُمْ قَدْ أَفْضَوْا إِلَى مَا قَدَّمُوا».
Maelezo ya hadith: Msiwatukane wafu, kwani wao tayari wameyapata yale wali…
Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- uharamu wa kuwatukana wafu na kuchafua heshima zao, nakuwa hili ni katika tabia mbaya, kwani wao wameyafikia yale waliyoyatanguliza katika matendo mazuri au mabaya, kama ambavyo matusi haya hayawafikii basi hakuna lolote zaidi ya kuwaudhi waliohai.
Mafunzo: Msiwatukane wafu, kwani wao tayari wameyapata yale wali…
- Hadithi ni ushahidi wa uharamu wa kuwatukana wafu.
- Kuacha kuwatukana wafu kuna kuchunga masilahi ya waliohai, na kuhifadhi amani ya jamii kutokana na kutotiliana vinyongo na chuki.
- Hekima ya kukatazwa kuwatukana nikuwa tayari wao wameyafikia yale waliyoyatanguliza, kuwatukana hakusaidii, na kuna kuwaudhi ndugu zake wa karibu.
- Nikuwa haifai kwa mwanadamu kusema maneno yasiyo na manufaa.
Makundi :
Fiq'hi- Ufahamu- wa Ibada mbalimbali.
· Majeneza.
· Fiq'hi na misingi yake.
· Mauti na Hukumu zake.
· Mambo mazuri na Adabu- Heshima.
بسم الله الرحمن الرحيم
mar. 15 Joumada 1
الثلاثاء 15 جمادى الأولى
اللهم صل على محمد
Ô Allah prie sur Muhammad