Nimeamrishwa nisujudu kwa viungo saba

Islam > Sw > Hadith > Fiqhi ufahamu wa ibada mbalimbali > Nimeamrishwa nisujudu kwa viungo saba

Hadith imesimuliwa na: Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake

Sahihi

Mis à jour le 26 octobre 2026

📖 1 min de lecture

Maandishi ya hadith: Nimeamrishwa nisujudu kwa viungo saba

Maelezo ya hadith: Nimeamrishwa nisujudu kwa viungo saba

Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa Mwenyezi Mungu kamuamrisha wakati wa swala asujudu kwa viungo saba katika viungo vya mwili; navyo ni:

Cha kwanza: Paji la uso: Nao ni ubapa wa uso ulioko juu ya pua na macho mawili, Na akaashiria -Rehema na amani ziwe juu yake- kwa mkono wake katika pua yake, akieleza kuwa paji la uso na pua ni kiungo kimoja katika vile saba, na akitia msisitizo kwa mwenye kusujudu kuwa agusishe pua yake katika ardhi.

Cha pili: na cha tatu: Ni mikono miwili.

Cha nne na cha tano: Ni magoti mawili.

Cha sita na cha saba: Ni vidole vya miguu miwili.

Na akatuamrisha tusizifunge nywele zetu, au kuzikunja kunja nguo zetu katika ardhi wakati wa kusujudu kwa kuilinda ardhi (Isiguse paji la uso); bali tuziache mpaka zidondoke katika ardhi, ili zisujudu pamoja viungo.

Mafunzo: Nimeamrishwa nisujudu kwa viungo saba

Makundi : Fiq'hi- Ufahamu- wa Ibada mbalimbali. · Sala. · Fiq'hi na misingi yake. · Sifa za Swala.

بسم الله الرحمن الرحيم mar. 15 Joumada 1
الثلاثاء 15 جمادى الأولى
بدر Pleine Lune Jour 16.6 / 29.5
Illumination 96%
Nouvelle lune dans 13 jours
الله أكبر Allah est le plus grand

إِنَّ ٱللَّهَ وَمَلَٰٓئِكَتَهُۥ يُصَلُّونَ عَلَى ٱلنَّبِىِّ ۚ يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ صَلُّوا۟ عَلَيْهِ وَسَلِّمُوا۟ تَسْلِيمًا

Al-Ahzab 33:56