Kwa hakika ima wakome watu kuziacha swala za Ijumaa, au Mwenyezi Mungu atawapiga mihuri ju…
Islam > Sw > Hadith > Fiqhi ufahamu wa ibada mbalimbali > Kwa hakika ima wakome watu kuziacha swala za Ijumaa, au Mwenyezi Mungu atawapiga mihuri ju…
Hadith imesimuliwa na: Imepokelewa Imamu Muslim
Sahihi
Mis à jour le 26 octobre 2026
📖 1 min de lecture
Maandishi ya hadith: Kwa hakika ima wakome watu kuziacha swala za Ijumaa, au…
Maelezo ya hadith: Kwa hakika ima wakome watu kuziacha swala za Ijumaa, au…
Amemtahadharisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake akiwa juu ya Mimbari yake, mwenye kuacha swala ya Ijumaa na kutohudhuria bila udhuru, kwa uvivu na uzembe, au vinginevyo Mwenyezi Mungu atapiga muhuri juu ya nyoyo zao na kuzifunika na kuziwekea kizuizi kitakachozizuia kufuata haki, kisha wawe miongoni mwa walioghafilika kuzikumbuka sababu za kheri, na kinachokataa kheri ni nafsi zao wao wenyewe.
Mafunzo: Kwa hakika ima wakome watu kuziacha swala za Ijumaa, au…
- Mkazo katika kuacha swala za Ijumaa, na kwamba hilo ni katika madhambi makubwa.
- Amesema Nawawi: Hapa ni kwamba Ijumaa ni faradhi kwa kila mmoja.
- Sheria ya kuweka Mimbari kwa ajili ya hotuba.
- Amesema Assanadi: Maana yake ni kwamba moja kati ya mambo ni lazima litokee hakuna namna, ima kukoma kuacha swala za Ijumaa, au Mwenyezi Mungu kupiga muhuri juu ya mioyo yao, kwani kuzoea kuacha Ijumaa hujaza mfuniko juu ya moyo, na kuiweka mbali nafsi na mambo ya ibada.
- Ni wajibu kwa mtoa mawaidha na mkumbushaji kuficha majina ya watu anaotaka kuwazungumzia katika mawaidha; kwa sababu hilo huleta msukumo zaidi wa kukubali nasaha, na kuzitekeleza amri.
Makundi :
Fiq'hi- Ufahamu- wa Ibada mbalimbali.
· Sala.
· Fiq'hi na misingi yake.
· Swala ya Ijumaa
· Virtue of Friday
بسم الله الرحمن الرحيم
mer. 16 Joumada 1
الأربعاء 16 جمادى الأولى
سبحان الله
Gloire à Allah