Mtu hawi na nguvu kwa kupigana miereka, bali mwenye nguvu ni yule anayeimiliki nafsi yake …
Islam > Sw > Hadith > Mambo mazuri na adabu heshima > Mtu hawi na nguvu kwa kupigana miereka, bali mwenye nguvu ni yule anayeimiliki nafsi yake …
Hadith imesimuliwa na: Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Sahihi
Mis à jour le 26 octobre 2026
📖 1 min de lecture
Maandishi ya hadith: Mtu hawi na nguvu kwa kupigana miereka, bali mwenye ngu…
عن أبي هريرة رضي الله عنه أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال: «لَيْسَ الشَّدِيدُ بِالصُّرَعَةِ، إِنَّمَا الشَّدِيدُ الَّذِي يَمْلِكُ نَفْسَهُ عِنْدَ الْغَضَبِ».
Maelezo ya hadith: Mtu hawi na nguvu kwa kupigana miereka, bali mwenye ngu…
Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa nguvu halisi si nguvu za mwili,au yule anayemdondosha mwenzake katika wenye nguvu, bali mwenye nguvu na mkali ni yule aliyepambana na nafsi yake na akaitenza nguvu wakati hasira inapokuwa kali; kwa sababu hili linaonyesha uwezo wa nguvu za kuidhibiti nafsi yake na kumshinda kwake Shetani.
Mafunzo: Mtu hawi na nguvu kwa kupigana miereka, bali mwenye ngu…
- Fadhila za upole na kudhibiti nafsi wakati wa hasira, nakuwa hili ni katika matendo mema ambayo uislamu umeyahimiza.
- Kupambana na nafsi wakati wa hasira ni zaidi ya kupambana na adui.
- Uislamu umebadili mtazamo wa nguvu wa enzi za ujinga kuwa ni tabia njema, hivyo, mtu mwenye nguvu zaidi kuliko wote ni yule mwenye kumiliki uongozi wa nafsi yake.
- Kujiweka mbali na hasira; kwani husababisha madhara kwa mtu mmoja mmoja na kwa jamii nzima kwa ujumla.
Makundi :
Fiq'hi ya Tabia.
· Tabia njema.
· Mambo mazuri na Adabu- Heshima.
بسم الله الرحمن الرحيم
mar. 15 Joumada 1
الثلاثاء 15 جمادى الأولى
أستغفر الله
Je demande pardon à Allah