Haingii peponi mkata udugu
Islam > Sw > Hadith > Mambo mazuri na adabu heshima > Haingii peponi mkata udugu
Hadith imesimuliwa na: Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Sahihi
Mis à jour le 26 octobre 2026
📖 1 min de lecture
Maandishi ya hadith: Haingii peponi mkata udugu
عن جُبَير بن مُطْعِم رضي الله عنه أنه سمع النبي صلى الله عليه وسلم يقول: «لَا يَدْخُلُ الْجَنَّةَ قَاطِعُ رَحِمٍ».
Maelezo ya hadith: Haingii peponi mkata udugu
Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yakuwa atakayewakatia ndugu zake wa karibu zile haki za wajibu kwao, au akawaudhi au kuwafanyia ubaya, basi anastahiki asiingie peponi.
Mafunzo: Haingii peponi mkata udugu
- Kukata udugu ni dhambi kubwa katika madhambi makubwa.
- Kuunga udugu kunakuwa kulingana na desturi za watu, na kutatofautiana kulingana na mazingira na zama na jamii pia.
- Kuunga udugu kunakuwa kwa kutembeleana, na kwa sadaka, na kuwatendea wema, na kuwatembelea wagonjwa, na kuwaamrisha mema, na kuwakataza maovu, na mengineyo.
- Kila ambavyo kukata udugu kunavyozidi kuwa kwa ndugu wa karibu zaidi ndivyo ambavyo madhambi yanavyokuwa makubwa.
Makundi :
Mambo yaliyo bora.
· Ubora wa kuunga udugu.
· Mambo mazuri na Adabu- Heshima.
بسم الله الرحمن الرحيم
mar. 15 Joumada 1
الثلاثاء 15 جمادى الأولى
أستغفر الله
Je demande pardon à Allah