Si halali kwa mwanamke wa kiislamu kusafiri mwendo wa usiku mmoja, isipokuwa awe pamoja na…
Islam > Sw > Hadith > Fiqhi ufahamu wa ibada mbalimbali > Si halali kwa mwanamke wa kiislamu kusafiri mwendo wa usiku mmoja, isipokuwa awe pamoja na…
Hadith imesimuliwa na: Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Sahihi
Mis à jour le 26 octobre 2026
📖 1 min de lecture
Maandishi ya hadith: Si halali kwa mwanamke wa kiislamu kusafiri mwendo wa u…
Maelezo ya hadith: Si halali kwa mwanamke wa kiislamu kusafiri mwendo wa u…
Amebainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa ni haramu kwa mwanamke wa kiislamu kusafiri mwendo wa usiku mmoja isipokuwa awe pamoja na mwanaume katika maharimu wake.
Mafunzo: Si halali kwa mwanamke wa kiislamu kusafiri mwendo wa u…
- Amesema bin Hajari: Kutofaa kwa mwanamke kusafiri pasina maharim (ndugu), ni makubaliano ya wanachuoni isipokuwa katika Hija na Umra, na kutoka katika mji wa ushirikina, na wako waliolifanya hilo kuwa ni katika masharti ya Hija.
- Ukamilifu wa sheria ya Uislamu, na pupa yake juu ya kumlinda mwanamke na kumchunga.
- Kumuamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho kunapelekea kunyenyekea sheria za Mwenyezi Mungu, na kusimama katika mipaka yake.
- Maharimu wa mwanamke ni mume wake au mtu wa haramu kwake kumuoa milele kwa sababu ya ukaribu wa kiukoo, au kunyonya, au ukwe, na anatakiwa awe muislamu, aliyebaleghe, mwenye akili timamu, mkweli, mwaminifu; kwa sababu lengo la maharimu ni kumlinda mwanamke na kumchunga na kusimamia mambo yake.
- Amesema Baihaqi: Kuhusu riwaya zilizokuja katika muda wa safari anaosafiri mwanamke ndani yake pamoja na maharimu: Na kilichopo nikuwa kila kinachoitwa safari mwanamke anakatazwa kusafiri pasina mume au maharimu, sawa sawa ziwe ni siku tatu au mbili au moja, au kaagizwa au kinginecho; kwa sababu ya riwaya ya bin Abbasi ambayo haikubagua, na ndio riwaya za mwisho za Imam Muslim zilizotangulia: "Asisafiri mwanamke isipokuwa awe pamoja na maharimu" Na hii inakusanya yote yanayoitwa safari. Mwisho, na hadithi hii ilikuwa kulingana na hali ya muulizaji na mji wake.
Makundi :
Fiq'hi- Ufahamu- wa Ibada mbalimbali.
· Hijja na Umra.
· Adabu za kisheria.
· Adabu na Hukumu za Safari.
· Fiq'hi na misingi yake.
· Mambo mazuri na Adabu- Heshima.
· Yaliyo wajibu katika Umra.
بسم الله الرحمن الرحيم
mar. 15 Joumada 1
الثلاثاء 15 جمادى الأولى
حسبنا الله ونعم الوكيل
Allah nous suffit, quel excellent protecteur