Wema ni tabia njema, na dhambi ni lile litakalokukereketa katika kifua chako, na ukachukia…

Islam > Sw > Hadith > Mambo mazuri na adabu heshima > Wema ni tabia njema, na dhambi ni lile litakalokukereketa katika kifua chako, na ukachukia…

Hadith imesimuliwa na: Imepokelewa Imamu Muslim

Sahihi

Mis à jour le 26 octobre 2026

📖 1 min de lecture

Maandishi ya hadith: Wema ni tabia njema, na dhambi ni lile litakalokukereke…

عَنِ النَّوَّاسِ بْنِ سِمْعَانَ الْأَنْصَارِيِّ رضي الله عنه قَالَ: سَأَلْتُ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَنِ الْبِرِّ وَالْإِثْمِ، فَقَالَ: «الْبِرُّ حُسْنُ الْخُلُقِ، وَالْإِثْمُ مَا حَاكَ فِي صَدْرِكَ، وَكَرِهْتَ أَنْ يَطَّلِعَ عَلَيْهِ النَّاسُ».

Maelezo ya hadith: Wema ni tabia njema, na dhambi ni lile litakalokukereke…

Aliulizwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuhusu wema na dhambi, akasema:

Kubwa kabisa katika wema ni tabia njema pamoja na Allah, kwa kumcha, na pamoja na watu, kwa kuvumilia kero, na kupunguza hasira, na kukunjua uso, na kuwa na maneno mazuri, na kuunga udugu na kutii na kuwa mpole na kutenda wema, na kuishi vizuri na familia, na kusuhubiana na watu vizuri.

Na ama dhambi ni kila kitakachokereketa ndani ya nafsi katika mambo yenye kutatiza, na kifua kikakosa utulivu na kutokunjuka, na moyo ukapata shaka, na ukaogoga kwa sababu ni dhambi, na ukawa hukutaka kulidhihirisha kwa mtu au hadharani mbele za watu kwakuwa ni baya, na hii ni kwa sababu nafsi hupenda watu waone yale mazuri yake, ikiwa itachukia watu kuyaona baadhi matendo yake basi hayo ndiyo madhambi wala hayana kheri ndani yake.

Mafunzo: Wema ni tabia njema, na dhambi ni lile litakalokukereke…

Makundi : Fiq'hi ya Tabia. · Tungo zenye kulainisha moyo na mawaidha · Tabia njema. · Matendo ya moyoni. · Mambo mazuri na Adabu- Heshima.

بسم الله الرحمن الرحيم mar. 15 Joumada 1
الثلاثاء 15 جمادى الأولى
بدر Pleine Lune Jour 16.6 / 29.5
Illumination 96%
Nouvelle lune dans 13 jours
الحمد لله Louange à Allah

إِنَّ ٱللَّهَ وَمَلَٰٓئِكَتَهُۥ يُصَلُّونَ عَلَى ٱلنَّبِىِّ ۚ يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ صَلُّوا۟ عَلَيْهِ وَسَلِّمُوا۟ تَسْلِيمًا

Al-Ahzab 33:56