Mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho basi na aseme la kheri au anyamaze

Islam > Sw > Hadith > Mambo mazuri na adabu heshima > Mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho basi na aseme la kheri au anyamaze

Hadith imesimuliwa na: Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake

Sahihi

Mis à jour le 26 octobre 2026

📖 1 min de lecture

Maandishi ya hadith: Mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho basi…

عن أبي هريرة رضي الله عنه عن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال: «مَنْ كَانَ يُؤْمِنُ بِاللهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ فَلْيَقُلْ خَيْرًا أَوْ لِيَصْمُتْ، وَمَنْ كَانَ يُؤْمِنُ بِاللهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ فَلْيُكْرِمْ جَارَهُ، وَمَنْ كَانَ يُؤْمِنُ بِاللهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ فَلْيُكْرِمْ ضَيْفَهُ».

Maelezo ya hadith: Mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho basi…

Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yakuwa mja mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho ambayo ndani yake kuna marejeo yake na malipo ya matendo yake, basi imani yake inamuhimiza kufanya mambo haya.

La kwanza: Kauli njema: Kama tasbihi (kusema: Sub-haanallah) na tahlili (Laa ilaaha illa llaah) na kuamrisha mema, na kukataza mabaya, na kuwasuluhisha watu, ikiwa hatofanya hivyo basi ashikamane na ukimya, na ajizuie na maudhi yake, na ahifadhi ulimi wake.

La pili: Kumkirimu jirani: Kwa kumtendea wema na kutomuudhi.

La tatu: Kumkirimu mgeni anayekuja kukutembelea: Kwa maneno mazuri na kumlisha chakula na mfano wa hayo.

Mafunzo: Mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho basi…

Makundi : Fiq'hi ya Tabia. · Tabia njema. · Mambo mazuri na Adabu- Heshima.

بسم الله الرحمن الرحيم mar. 15 Joumada 1
الثلاثاء 15 جمادى الأولى
بدر Pleine Lune Jour 16.5 / 29.5
Illumination 97%
Nouvelle lune dans 13 jours
سبحان الله Gloire à Allah

إِنَّ ٱللَّهَ وَمَلَٰٓئِكَتَهُۥ يُصَلُّونَ عَلَى ٱلنَّبِىِّ ۚ يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ صَلُّوا۟ عَلَيْهِ وَسَلِّمُوا۟ تَسْلِيمًا

Al-Ahzab 33:56