Je mnajua ni nani aliyefilisika?

Islam > Sw > Hadith > Fiqhi ya tabia > Je mnajua ni nani aliyefilisika?

Hadith imesimuliwa na: Imepokelewa Imamu Muslim

Sahihi

Mis à jour le 26 octobre 2026

📖 1 min de lecture

Maandishi ya hadith: Je mnajua ni nani aliyefilisika?

Maelezo ya hadith: Je mnajua ni nani aliyefilisika?

Mtume rehema na amani ziwe juu yake aliwauliza Maswahaba zake: Je, mnamjua aliyefilisika? Wakasema: Aliyefilisika miongoni mwetu ni yule asiye na fedha wala mali. Akasema: Aliyefilisika katika umma wangu Siku ya Kiyama ni yule anayefanya mambo mema kama Swala, Saumu na Zaka, na akaja akiwa kamshutumu huyu na kamtukana huyu, na kamsingizia mabaya mtu huyu katika heshima yake, na kala mali ya huyu na akakana, na akamwaga damu ya huyu na kumdhulumu, na kampiga huyu na akamdhalilisha, hivyo mtu aliyedhulumiwa atapewa kutoka katika matendo yake mema, mema yake yakimalizika kabla ya haki za watu na dhulma hazijamalizika, yatachukuliwa madhambi ya wale aliowadhulumu na kuwekwa katika vitabu vya dhalimu, kisha atatupwa na kurushwa motoni kwani hajabaki na jema.

Mafunzo: Je mnajua ni nani aliyefilisika?

Makundi : Fiq'hi ya Tabia. · Tabia mbovu. · Akida- Itikadi- · Mambo mazuri na Adabu- Heshima. · Kuamini siku ya mwisho · Maisha ya Akhera.

بسم الله الرحمن الرحيم mar. 15 Joumada 1
الثلاثاء 15 جمادى الأولى
بدر Pleine Lune Jour 16.5 / 29.5
Illumination 97%
Nouvelle lune dans 13 jours
الله أكبر Allah est le plus grand

إِنَّ ٱللَّهَ وَمَلَٰٓئِكَتَهُۥ يُصَلُّونَ عَلَى ٱلنَّبِىِّ ۚ يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ صَلُّوا۟ عَلَيْهِ وَسَلِّمُوا۟ تَسْلِيمًا

Al-Ahzab 33:56