Hivi nikuelezeni madhambi makubwa?

Islam > Sw > Hadith > Mambo mazuri na adabu heshima > Hivi nikuelezeni madhambi makubwa?

Hadith imesimuliwa na: Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake

Sahihi

Mis à jour le 26 octobre 2026

📖 1 min de lecture

Maandishi ya hadith: Hivi nikuelezeni madhambi makubwa?

عن أبي بكرة رضي الله عنه قال: قال النبي صلى الله عليه وسلم: «‌أَلَا ‌أُنَبِّئُكُمْ بِأَكْبَرِ الْكَبَائِرِ؟» ثَلَاثًا، قَالُوا: بَلَى يَا رَسُولَ اللهِ، قَالَ: «الْإِشْرَاكُ بِاللهِ، وَعُقُوقُ الْوَالِدَيْنِ» وَجَلَسَ وَكَانَ مُتَّكِئًا، فَقَالَ: «أَلَا وَقَوْلُ الزُّورِ»، قَالَ: فَمَا زَالَ يُكَرِّرُهَا حَتَّى قُلْنَا: لَيْتَهُ سَكَتَ.

Maelezo ya hadith: Hivi nikuelezeni madhambi makubwa?

Anawaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- Masahaba zake kuhusu madhambi makubwa, akataja haya matatu:

1- Ni kumshirikisha Mwenyezi Mungu: Nako ni kuielekeza aina yoyote katika aina za ibada kwa asiye Allah, na kumfanya kuwa sawa na Allah asiyekuwa Allah katika uungu wake na uumbaji na ulezi wake na majina yake na sifa zake.

2- Kuwaasi wazazi wawili: Nayo ni kila aina ya maudhi kwa wazazi wawili, sawa sawa iwe kwa kauli au kitendo, na kuacha kuwafanyia wema.

3- Kauli ya uongo ikiwemo ushahidi wa uongo: Nayo ni kila kauli ya kuzusha ya uongo, yenye lengo la kumdhalilisha yule anayekusudiwa kwa kuchukua mali yake au kumfanyia uadui katika heshima yake au mfano wa hayo.

Alikariri Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- tahadhari hii ya kusema uongo ikiwa ni tahadhari juu ya ubaya wake na athari zake mbaya kwa jamii, mpaka wakasema Masahaba: Laiti angelinyamaza; Kwa sababu ya kumhurumia, na kwa kuchukia kile kinachompa kero Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-.

Mafunzo: Hivi nikuelezeni madhambi makubwa?

Makundi : Fiq'hi ya Tabia. · Tungo zenye kulainisha moyo na mawaidha · Tabia mbovu. · Kuyasema vibaya Maasi. · Mambo mazuri na Adabu- Heshima.

بسم الله الرحمن الرحيم mar. 15 Joumada 1
الثلاثاء 15 جمادى الأولى
بدر Pleine Lune Jour 16.5 / 29.5
Illumination 96%
Nouvelle lune dans 13 jours
حسبنا الله ونعم الوكيل Allah nous suffit, quel excellent protecteur

إِنَّ ٱللَّهَ وَمَلَٰٓئِكَتَهُۥ يُصَلُّونَ عَلَى ٱلنَّبِىِّ ۚ يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ صَلُّوا۟ عَلَيْهِ وَسَلِّمُوا۟ تَسْلِيمًا

Al-Ahzab 33:56