Islam > Sw > Hadith > Mambo mazuri na adabu heshima > Mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho basi na aseme la kheri au anyamaze
SahihiMis à jour le 26 octobre 2026
📖 1 min de lectureعن أبي هريرة رضي الله عنه عن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال: «مَنْ كَانَ يُؤْمِنُ بِاللهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ فَلْيَقُلْ خَيْرًا أَوْ لِيَصْمُتْ، وَمَنْ كَانَ يُؤْمِنُ بِاللهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ فَلْيُكْرِمْ جَارَهُ، وَمَنْ كَانَ يُؤْمِنُ بِاللهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ فَلْيُكْرِمْ ضَيْفَهُ».
Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yakuwa mja mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho ambayo ndani yake kuna marejeo yake na malipo ya matendo yake, basi imani yake inamuhimiza kufanya mambo haya.
La kwanza: Kauli njema: Kama tasbihi (kusema: Sub-haanallah) na tahlili (Laa ilaaha illa llaah) na kuamrisha mema, na kukataza mabaya, na kuwasuluhisha watu, ikiwa hatofanya hivyo basi ashikamane na ukimya, na ajizuie na maudhi yake, na ahifadhi ulimi wake.
La pili: Kumkirimu jirani: Kwa kumtendea wema na kutomuudhi.
La tatu: Kumkirimu mgeni anayekuja kukutembelea: Kwa maneno mazuri na kumlisha chakula na mfano wa hayo.
Makundi : Fiq'hi ya Tabia. · Tabia njema. · Mambo mazuri na Adabu- Heshima.