Hakika mtu anayechukiza zaidi kwa Mwenyezi Mungu ni mgomvi mkorofi
Islam > Sw > Hadith > Mambo mazuri na adabu heshima > Hakika mtu anayechukiza zaidi kwa Mwenyezi Mungu ni mgomvi mkorofi
Hadith imesimuliwa na: Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Sahihi
Mis à jour le 26 octobre 2026
📖 1 min de lecture
Maandishi ya hadith: Hakika mtu anayechukiza zaidi kwa Mwenyezi Mungu ni mgo…
عن عائشة رضي الله عنها عن النبي صلى الله عليه وسلم قال: «إِنَّ أَبْغَضَ الرِّجَالِ إِلَى اللهِ الْأَلَدُّ الْخَصِمُ».
Maelezo ya hadith: Hakika mtu anayechukiza zaidi kwa Mwenyezi Mungu ni mgo…
Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa Mwenyezi Mungu -Aliyetakasika na kutukuka- anawachukia miongoni mwa watu mwenye ugomvi mkali na mwingi, asiyekubali kutii haki, na anajaribu kuikataa kwa mijadala, au akagombana kwa haki akapitiliza katika ugomvi na akatoka katika mpaka wa uadilifu, na akajadiliana bila elimu.
Mafunzo: Hakika mtu anayechukiza zaidi kwa Mwenyezi Mungu ni mgo…
- Haingii katika mlango wa mgomvi mbaya, aliyedhulumiwa kudai haki yake kwa njia ya kushitakiana kisheria.
- Mijadala na ugomvi ni katika maafa ya ulimi yanayosababisha kutengana na kupeana migongo kati ya waislamu.
- Mjadala ni mzuri utapokuwa katika haki na utaratibu mzuri, na unakuwa mbaya utapokuwa ni kwa kuikataa haki na kuitetea batili, au ukawa bila hoja wala ushahidi.
Makundi :
Fiq'hi ya Tabia.
· Tabia mbovu.
· Mambo mazuri na Adabu- Heshima.
بسم الله الرحمن الرحيم
mar. 15 Joumada 1
الثلاثاء 15 جمادى الأولى
لا إله إلا الله
Pas de divinité sauf Allah