Yaepukeni mambo saba yenye kuangamiza

Islam > Sw > Hadith > Mambo mazuri na adabu heshima > Yaepukeni mambo saba yenye kuangamiza

Hadith imesimuliwa na: Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake

Sahihi

Mis à jour le 26 octobre 2026

📖 2 min de lecture

Maandishi ya hadith: Yaepukeni mambo saba yenye kuangamiza

عن أبي هريرة رضي الله عنه عن النبي صلى الله عليه وسلم قال: «اجْتَنِبُوا السَّبْعَ الْمُوبِقَاتِ»، قَالُوا: يَا رَسُولَ اللهِ وَمَا هُنَّ؟ قَالَ: «الشِّرْكُ بِاللهِ، وَالسِّحْرُ، وَقَتْلُ النَّفْسِ الَّتِي حَرَّمَ اللهُ إِلَّا بِالْحَقِّ، وَأَكْلُ الرِّبَا، وَأَكْلُ مَالِ الْيَتِيمِ، وَالتَّوَلِّي يَوْمَ الزَّحْفِ، وَقَذْفُ الْمُحْصَنَاتِ الْمُؤْمِنَاتِ الْغَافِلَاتِ».

Maelezo ya hadith: Yaepukeni mambo saba yenye kuangamiza

Anaamrisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- umma wake kujitenga mbali na maovu saba na maasi yenye kuangamiza, na alipoulizwa ni yapi hayo? akayabainisha kuwa ni:

La kwanza: Ni kumshirikisha Mwenyezi Mungu na kitu kingine, kwa kujifanyia mshirika na mfano wake utakasifu ni wake kwa namna yoyote ile itakayokuwa, na kuielekeza aina yoyote ya ibada miongoni mwa ibada kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kaanza na ushirikina; kwa sababu ndio dhambi kubwa kuliko yote.

La pili: Uchawi -Nao namna ya ufungaji mafundo na makombe na madawa na ufukishaji mioshi-, yanayoleta athari katika mwili wa mwenye kurogwa kwa kuua au kutia maradhi, au kuwatenganisha kati ya wana ndoa wawili, nayo ni kazi ya kishetani, na wengi wao hawaufikii uchawi isipokuwa kwa ushirikina na kujikurubisha kwa maruhani wachafu kwa kitu wanachokipenda.

La tatu: Ni kuua nafsi aliyokataza Allah isiuliwe isipokuwa kwa kigezo cha kisheria, na hutekelezwa na hakimu.

La nne: Kutumia riba kwa kula au kwa njia nyingine katika njia za kunufaika.

La tano: Kufanya uadui katika mali ya mtoto mdogo aliyefiwa na baba yake naye akiwa chini ya umri wa kubalehe.

La sita: Kukimbia katika vita kati ya waislamu na makafiri.

La saba: Kuwatuhumu wanawake huru wenye kujizuia na machafu kwa uzinifu, na vile vile kuwatuhumu wanaume.

Mafunzo: Yaepukeni mambo saba yenye kuangamiza

Makundi : Fiq'hi ya Tabia. · Tungo zenye kulainisha moyo na mawaidha · Tabia mbovu. · Kuyasema vibaya Maasi. · Mambo mazuri na Adabu- Heshima.

بسم الله الرحمن الرحيم mar. 15 Joumada 1
الثلاثاء 15 جمادى الأولى
بدر Pleine Lune Jour 16.5 / 29.5
Illumination 96%
Nouvelle lune dans 13 jours
أستغفر الله Je demande pardon à Allah

إِنَّ ٱللَّهَ وَمَلَٰٓئِكَتَهُۥ يُصَلُّونَ عَلَى ٱلنَّبِىِّ ۚ يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ صَلُّوا۟ عَلَيْهِ وَسَلِّمُوا۟ تَسْلِيمًا

Al-Ahzab 33:56