Tahadharini na dhana; kwani dhana ni mazungumzo ya uongo mno

Islam > Sw > Hadith > Fiqhi ya tabia > Tahadharini na dhana; kwani dhana ni mazungumzo ya uongo mno

Hadith imesimuliwa na: Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake

Sahihi

Mis à jour le 26 octobre 2026

📖 1 min de lecture

Maandishi ya hadith: Tahadharini na dhana; kwani dhana ni mazungumzo ya uong…

Maelezo ya hadith: Tahadharini na dhana; kwani dhana ni mazungumzo ya uong…

Anakataza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- na anatahadharisha baadhi ya yale yanayoweza kupelekea kufarakana na uadui baina ya waislamu, na miongoni mwayo:

(Dhana) Nazo ni tuhuma zinazojitokeza ndani ya moyo pasina ushahidi, na akabainisha kuwa hayo ni mazungumzo ya uongo mno.

Na kuhusu (kuhisiana vibaya): Nako ni kutafuta aibu za watu kwa kutazama au kusikiliza.

(Na kupelelezana): Nako ni kutafuta yaliyofichikana miongoni mwa mambo, na hii hutumika zaidi katika shari.

Na kuhusu: (Husuda) nako ni kuchukia kupatikana kwa neema kwa watu wengine.

Na kuhusu (Kutengana) kwa kuwapuuza baadhi ya watu wenzao, hamsalimii wala hamtembelei ndugu yake muislamu,

Na kuhusu: (Kuchukiana) na kuchukia na kubeza, kama kuwaudhi watu wengine, na kutotabasamu, na kukutana nao kwa sura mbaya.

Kisha akazungumza neno moja linalokusanya kila kitu, ambalo litatengeneza hali za waislamu baadhi yao kwa baadhi: (Na kuweni waja wa Mwenyezi Mungu ndugu wamoja). Udugu ni kiunganishi kinachounganisha mahusiano kati ya watu, na kinazidisha mapenzi na kuzoeana baina yao.

Mafunzo: Tahadharini na dhana; kwani dhana ni mazungumzo ya uong…

Makundi : Fiq'hi ya Tabia. · Tabia mbovu. · Mambo mazuri na Adabu- Heshima.

بسم الله الرحمن الرحيم mar. 15 Joumada 1
الثلاثاء 15 جمادى الأولى
بدر Pleine Lune Jour 16.5 / 29.5
Illumination 96%
Nouvelle lune dans 13 jours
لا حول ولا قوة إلا بالله Pas de force ni de puissance sauf en Allah

إِنَّ ٱللَّهَ وَمَلَٰٓئِكَتَهُۥ يُصَلُّونَ عَلَى ٱلنَّبِىِّ ۚ يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ صَلُّوا۟ عَلَيْهِ وَسَلِّمُوا۟ تَسْلِيمًا

Al-Ahzab 33:56