Hakika watoa laana hawatokuwa mashahidi wala watetezi siku ya Kiyama
Islam > Sw > Hadith > Fiqhi ya tabia > Hakika watoa laana hawatokuwa mashahidi wala watetezi siku ya Kiyama
Hadith imesimuliwa na: Imepokelewa Imamu Muslim
Sahihi
Mis à jour le 26 octobre 2026
📖 1 min de lecture
Maandishi ya hadith: Hakika watoa laana hawatokuwa mashahidi wala watetezi s…
Maelezo ya hadith: Hakika watoa laana hawatokuwa mashahidi wala watetezi s…
Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa mwenye kukithirisha laana kwa mtu asiyestahiki huyu anastahiki kupata adhabu mbili. Ya kwanza: Hatokuwa shahidi siku ya Kiyama juu ya umma kwa mitume wao kufikisha ujumbe kwao, na wala haukubaliki ushahidi wake duniani; kwa sababu ya uovu wake, na wala hatoruzukiwa shahada, nako ni kufa katika njia ya Mwenyezi Mungu. Ya pili: Hatopewa nafasi ya kutoa utetezi siku ya Kiyama wakati ambapo waumini wataomba utetezi kwa ndugu zao waliostahiki moto.
Mafunzo: Hakika watoa laana hawatokuwa mashahidi wala watetezi s…
- Uharamu wa kutoa laana, nakuwa kukithirisha hilo ni dhambi miongoni mwa madhambi makubwa.
- Adhabu iliyotajwa katika hadithi inamuhusu anayekithirisha kulaani, si wa mara moja na mfano wake, kwa sababu kwake pia kunatoka laana za halali, nazo ni zile ambazo sheria imekuja kuwalaani watu wenye sifa mbaya pasina kumuainisha mtu, kama kusema: "Mwenyezi Mungu awalaani Mayahudi na Wakristo", "Laana za Mwenyezi Mungu ziwe juu ya madhalimu" Mwenyezi Mungu amewalaani wanaopiga picha", "Mwenyezi Mungu amemlaani atakayefanya vitendo vya watu wa Luti", "Mwenyezi Mungu amemlaani atakayechinja kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu", "Mwenyezi Mungu amewalaani wanaume wenye kujifananisha na wanawake, na wanawake wenye kujifananisha na wanaume", na mfano wa hizo.
- Kumethibitishwa uombezi wa waumini siku ya Kiyama.
Makundi :
Fiq'hi ya Tabia.
· Tabia mbovu.
· Mambo mazuri na Adabu- Heshima.
بسم الله الرحمن الرحيم
mar. 15 Joumada 1
الثلاثاء 15 جمادى الأولى
لا إله إلا الله
Pas de divinité sauf Allah