Hakika Mwenyezi Mungu huwaadhibu wale wanaowaadhibu watu duniani
Islam > Sw > Hadith > Fiqhi ya tabia > Hakika Mwenyezi Mungu huwaadhibu wale wanaowaadhibu watu duniani
Hadith imesimuliwa na: Imepokelewa Imamu Muslim
Sahihi
Mis à jour le 26 octobre 2026
📖 1 min de lecture
Maandishi ya hadith: Hakika Mwenyezi Mungu huwaadhibu wale wanaowaadhibu wat…
Maelezo ya hadith: Hakika Mwenyezi Mungu huwaadhibu wale wanaowaadhibu wat…
Alipita Hisham bin Hakim bin Hizam radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao, kwa wakulima wasiokuwa Waarabu huko Sham, wakiwa wamesimamishwa chini ya joto la Jua, akauliza kuhusu jambo lililowapata? Akaambiwa kuwa wamefanywa hivyo kwa sababu ya kutolipa Jizia (kodi) hali yakuwa wanauwezo wa kulipa. Amesema Hisham radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: Ninashuhudia kuwa hakika nilimsikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake akisema: Hakika Mwenyezi Mungu huwaadhibu wale wanaowaadhibu watu duniani kwa dhuluma pasina haki.
Mafunzo: Hakika Mwenyezi Mungu huwaadhibu wale wanaowaadhibu wat…
- Jizia: Ni mali inayowekwa kuwa sheria kwa wanaume miongoni mwa Mayahudi na Manaswara waliobalehe wenye uwezo, kwa ajili ya kulindwa kwao na kuishi kwao katika mji wa kiislamu.
- Uharamu wa kuwaadhibu watu hata makafiri, pasina kigezo cha kisheria.
- Onyo kwa madhalimu kutokana na dhuluma.
- Walishikamana Maswahaba wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake na kuamrisha mema na kukataza maovu.
- Amesema Nawawi: Hii inachukuliwa katika kuadhibu bila haki, haiingii kuadhibu kwa haki kama kisasi, na kusimamishiwa sheria, na kuonya, na mfano wake.
Makundi :
Fiq'hi ya Tabia.
· Tabia mbovu.
· Mambo mazuri na Adabu- Heshima.
بسم الله الرحمن الرحيم
mar. 15 Joumada 1
الثلاثاء 15 جمادى الأولى
لا إله إلا الله
Pas de divinité sauf Allah