Islam > Sw > Hadith > Mambo mazuri na adabu heshima > Allah amhurumie mtu ambaye ni mpole anapouza, na anaponunua, na anapo dai deni
SahihiMis à jour le 26 octobre 2026
📖 1 min de lectureعن جابر رضي الله عنه أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال: «رَحِمَ اللهُ رَجُلًا سَمْحًا إِذَا بَاعَ، وَإِذَا اشْتَرَى، وَإِذَا اقْتَضَى».
Alimuombea rehema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kila mwenye kuwa mwepesi mkarimu mpole katika biashara yake; Hamkadamizi mnunuzi katika bei yake, na anaamiliana naye kwa tabia njema, Mwepesi mkarimu mpole anaponunua; Hapunji na kupunguza thamani ya bidhaa, Mwepesi mkarimu mpole anapodai kulipwa madeni yake; hamtilii mkazo fukara na muhitaji, bali anamdai kwa upole na huruma, na anampa muda mwenye hali ngumu.
Makundi : Fiq'hi ya Tabia. · Tabia njema. · Mambo mazuri na Adabu- Heshima.