Atakayejifunza elimu katika yale yanayo ambayo hutafutwa radhi za Mwenyezi Mungu Mtukufu, …
Islam > Sw > Hadith > Fiqhi ya tabia > Atakayejifunza elimu katika yale yanayo ambayo hutafutwa radhi za Mwenyezi Mungu Mtukufu, …
Hadith imesimuliwa na: Imepokelewa na Abu Daud, Ibn Majah na Ahmad
Sahihi
Mis à jour le 26 octobre 2026
📖 1 min de lecture
Maandishi ya hadith: Atakayejifunza elimu katika yale yanayo ambayo hutafutw…
Maelezo ya hadith: Atakayejifunza elimu katika yale yanayo ambayo hutafutw…
Amebainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kwamba atakayejifunza elimu ya kisheria ambayo asili yake ni kutafutwa radhi za Mwenyezi Mungu Mtukufu, hajifunzi isipokuwa apate heshima na starehe za kidunia miongoni mwa mali au cheo, basi hatoipata harufu ya Pepo siku ya Kiyama.
Mafunzo: Atakayejifunza elimu katika yale yanayo ambayo hutafutw…
- Uwajibu wa kutakasa nia katika kutafuta elimu, na himizo juu ya hilo.
- Tahadhari kubwa ya kuichukua elimu ya kisheria kwa kujionyesha au daraja la kuifikia dunia, na kwamba hilo ni katika madhambi makubwa.
- Nikuwa atakayeitafuta elimu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu na ikamuijia dunia yenyewe inafaa kwake kuichukua, na hilo halitomdhuru.
- Amesema Assanadi: Kauli yake: "Harufu ya Pepo" Neno harufu limetumika likiashiria kupita kiasi katika kuharamishwa Pepo; kwa sababu asiyeweza kupata harufu ya kitu hawezi kukipata.
- Atakayejifunza elimu katika yale ambayo hutafutwa radhi za Mwenyezi Mungu kwayo, kwa ajili ya kupata ajira, au kwa ajili ya malengo mengine; basi anatakiwa kutubia kwa Mwenyezi Mungu kutokana na hilo, na Mwenyezi Mungu atamfutia yaliyojitokeza miongoni mwa nia mbaya, kwani Yeye anafadhila kubwa Aliyetakasika na kutukuka.
- Tahadhari hii ni kwa mwenye kutafuta elimu ya kisheria, ama atakayetafuta elimu yoyote katika elimu za kidunia kwa ajili ya starehe za dunia, kama uhandisi, na kemia, na mengineyo kwa ajili ya masilahi ya dunia, hakuna shaka atalipwa kwa nia yake.
Makundi :
Fiq'hi ya Tabia.
· Adabu za kisheria.
· Tabia mbovu.
· Adabu za mjuzi na mwenye kujifunza.
· Mambo mazuri na Adabu- Heshima.
بسم الله الرحمن الرحيم
mar. 15 Joumada 1
الثلاثاء 15 جمادى الأولى
لا إله إلا الله
Pas de divinité sauf Allah