Hadith kuhusu Mambo mazuri na Adabu- Heshima.

Islam > Sw > Hadith > Mambo mazuri na Adabu- Heshima.

Hadith 386 za Nabii zilizoelezwa kuhusu «Mambo mazuri na Adabu- Heshima.»: maandishi ya Kiarabu, tafsiri, maelezo na mafunzo, na kiwango cha ukweli na vyanzo.

Mis à jour le 26 octobre 2026

Orodha ya hadith kuhusu Mambo mazuri na Adabu- Heshima.

Sahihi Mtu hawi na nguvu kwa kupigana miereka, bali mwenye nguvu ni yule anayeimiliki nafsi yake wakati wa hasira Sahihi Atakayeelekeza katika jambo la kheri basi atapata malipo mfano wa malipo ya mfanyaji wake Sahihi Msiwatukane wafu, kwani wao tayari wameyapata yale waliyoyatanguliza Sahihi Ni haramu kwa mtu kumhama ndugu yake zaidi ya siku tatu, wanakutana, huyu akampuuza huyu na huyu naye akampuuza huyu, na mbora wao ni yule anaye anza Sahihi Haingii peponi mkata udugu Sahihi Haingii peponi mfitinishaji Sahihi Hamtazami Mwenyezi Mungu mwenye kuburuza nguo yake kwa kiburi Sahihi Hakuna kitu chenye uzito zaidi katika mizani ya muumini siku ya Kiyama kuliko tabia njema, na hakika Mwenyezi Mungu anamchukia mtu muovu mwenye kauli Sahihi Atakayependa kukunjuliwa katika riziki yake, na acheleweshewe ajali yake, basi na aunge udugu wake Sahihi Hakika Mtume rehema na amani ziwe juu yake alitoka kwetu sisi, tukasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, tumekwishafahamu ni vipi tutakusalimu, sasa ni Sahihi Palipo karibu zaidi kwa mja na Mola wake ni pale anapokuwa kasujudu,Basi zidisheni dua Sahihi Bahili ni yule ambaye nitatajwa mbele yake, akawa hakuniswalia Ni nzuri (Hasan) Atakayekula chakula, akasema: Kila sifa njema zinamstahiki Mwenyezi Mungu aliyenilisha chakula hiki, na akaniruzuku, si kwa ujanja wangu wala kwa nguv Sahihi Mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho basi na aseme la kheri au anyamaze Sahihi Asiyewahurumia watu naye Mwenyezi Mungu Mtukufu hamhurumii Sahihi Neema mbili wamepoteza thamani yake watu wengi: Afya na wakati Ni nzuri (Hasan) “Ewe mwanadam, maadamu unaniomba na kunitumainia, nitakusamehe uliyo nayo wala sitojali Sahihi Yakwamba Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- alikuwa akisema katika sijida yake: "Ewe Mwenyezi Mungu nisamehe mimi dhambi zangu ndogo zake na kubwa Sahihi Hakika mtu anayechukiza zaidi kwa Mwenyezi Mungu ni mgomvi mkorofi Sahihi Maneno yanayopendeka zaidi kwa Allah ni manne: Sub-haanallah, Al-hamdulillaah, na Laa ilaaha illa llaah, na Allahu Akbar, haidhuru ikiwa utaanza na lo Ni nzuri (Hasan) na ni sahihi Aliulizwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuhusu mambo yatakayowaingiza watu peponi kwa wingi, akasema: "Ni uchamungu na tabia njema Sahihi Haya ni katika imani Sahihi Dua hairejeshwi (inayoombwa) baina ya adhana na kukimiwa swala Sahihi Ewe Mwenyezi Mungu nitengenezee dini yangu ambayo ndiyo kinga ya jambo langu Sahihi Ewe Mola wangu Mlezi nisamehe mimi makosa yangu, na ujinga wangu, na ubadhirifu wangu katika jambo langu lote, na yale unayoyajua kutoka kwangu, ewe M Sahihi Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninakuomba unipe afya katika Dunia na Akhera Sahihi Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninakuomba (unipe) kutoka katika heri zote: zile za haraka na za kuchelewa, kwa ninayo yajua na nisiyo yajua, na ninaji Sahihi Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi najikinga kwako kutokana na kuondokewa neema zako, na kubadilika kwa afya yako, na kufikiwa ghafla na adhabu zako, na k Sahihi Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninajikinga kwako kutokana na kushindwa kulipa deni, na kushindwa na maadui, na kutukanwa na maadui Ni nzuri (Hasan) Ewe Mwenyezi Mungu kwako tumeamka, na kwako tunashinda, na kwako tunakuwa hai, na kwako tutakufa, na kwako tutafufuliwa Sahihi Muumini mwenye nguvu ni bora na anapendeka kwa Mwenyezi Mungu kuliko muumini dhaifu, na katika kila kheri, Sahihi Hakika watoa laana hawatokuwa mashahidi wala watetezi siku ya Kiyama Sahihi Dua ndio ibada Sahihi Na hakika Mwenyezi Mungu ameniteremshia wahyi kuwa, kuweni wanyenyevu, mpaka asijikweze yeyote kwa mwingine, na wala asimfanyie uadui yeyote mwenzake Ni nzuri (Hasan) Hakika Mola wenu Mlezi ni Mwenye haya Mkarimu, anamuonea haya mja wake atakapo nyanyua mikono yake kumuelekezea kisha amrejeshe patupu Sahihi Ilikuwa Dua aiombayo zaidi Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake-:ni "Ewe Mola wetu Mlezi, tupe duniani mazuri, na Akhera mazuri, na utukinge na adha Sahihi Bwana wa Istighfari (Dua ya kuomba msamaha) Sahihi Kutoka kwa Abdillah bin Mas'udi -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Shikamaneni na ukweli Sahihi Maneno mawili mepesi mno katika ulimi, ni mazito mno katika mizani, yanapendeka mno kwa Al-Rahmani (Mwingi wa rehema) Sahihi Hakika ungesema maneno manne, mara tatu, kama ungeyapima kwa uliyo yasema toka siku ya leo yangeyazidi uzito Ni nzuri (Hasan) Hakuna kitu kinachotukuzwa zaidi kwa Allah Mtukufu kuliko dua Sahihi Hawajawahi kukaa watu kikao chochote wakawa hawakumtaja Mwenyezi Mungu ndani yake, na wala hawakumsalia Nabii wao, isipokuwa itakuwa ni hasara juu yao Sahihi Atakayeitetea heshima ya ndugu yake basi Mwenyezi Mungu ataukinga uso wake na moto siku ya Kiyama Sahihi Atakayesema: Sub-haanallahi wabihamdihi, (Ametakasika Mwenyezi Mungu na sifa njema ni zake) kwa siku mara mia moja (100), yatafutwa madhambi yake hata Sahihi Atakayesema: Laa ilaaha illa llaahu wahdahu Laa shariika lahu, Lahul-Mulku walahul hamdu Wahuwa a'laa kulli shai-in qadiir, mara kumi (10) Sahihi Mwenye kutakiwa kheri na Allah humpa ufahamu katika dini Sahihi Enyi watu, toleaneni salamu na muunge udugu, na mlishe chakula, na msali usiku watu wakiwa wamelala, mtaingia peponi kwa amani Sahihi Ondosha tatizo, ewe Mola wa watu, na ponya kwani wewe ndiye mponyaji, hakuna ponyo ila ponyo lako, ponyo lisiloacha ugonjwa Sahihi Hakika Mwenyezi Mungu humpenda mja mchamungu, mwenye kutosheka, mnyenyekevu Sahihi Hakika mfano wa mtu wa Qur'ani ni sawa na mfano wa mmiliki wa ngamia aliyeachwa pasina kufungwa, akimuangalia kila mara atamzuia (kutoroka), na akimua Sahihi Yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alikuwa hakatai marashi Sahihi Ogopeni dhulma, kwa hakika dhulma ni giza siku ya kiyama. Na ogopeni tamaa, kwa hakika tamaa iliwaangamiza walio kuwepo kabla yenu Ni nzuri (Hasan) Muumini iliyekamilika zaidi imani yake ni yule mwenye tabia nzuri zaidi kuliko wengine, na mbora wenu ni yule mbora wenu kwa wake zake Sahihi Hakika upole hauwi ndani ya kitu isipokuwa hukipendezesha, na hautolewi ndani ya kitu ila hukichafua Sahihi Ewe Aisha, hakika Mwenyezi Mungu ni Mpole anapenda upole, na hutoa malipo katika upole ambayo hayatoi katika ususuwavu (ukali), na wala hatoi kwa meng Sahihi Hakika Allah humridhia mja anapokula chakula akamshukuru juu ya chakula hicho, au akanywa kinywaji chochote akamshukuru kwa kinywaji hicho Ni sahihi kwa ushahidi wake mbalimbali Hakika muumini hufikia kwa sababu ya tabia zake njema daraja ya mfungaji mwenye kusimama usiku Sahihi Hakika kwako wewe kuna mambo mawili anayapenda sana Mwenyezi Mungu: Upole, na utaratibu Sahihi Hakika katika watu wanaopendeka zaidi kati yenu kwangu mimi, na atakayekaa karibu zaidi kati yenu na mimi siku ya Kiyama ni yule atakayekuwa na tabia Sahihi Hakika katika wabora wenu ni mtu mwenye tabia njema kuliko wote
بسم الله الرحمن الرحيم mer. 16 Joumada 1
الأربعاء 16 جمادى الأولى
أحدب متناقص Gibbeuse Décroissante Jour 17.4 / 29.5
Illumination 92%
Nouvelle lune dans 12 jours
الله أكبر Allah est le plus grand

إِنَّ ٱللَّهَ وَمَلَٰٓئِكَتَهُۥ يُصَلُّونَ عَلَى ٱلنَّبِىِّ ۚ يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ صَلُّوا۟ عَلَيْهِ وَسَلِّمُوا۟ تَسْلِيمًا

Al-Ahzab 33:56